
“Mjadala mkali mitandaoni kuhusu umiliki wa ardhi Zanzibar kwa Mtanzania anaetokea Bara, Mwandishi wa makala hii ni nguli wa uchambuzi wa masuala ya kisiasa kimataifa na masuala ya kijamii Ndugu Harid Mkali ametoa angalizo dogo muhimu baada ya mjadala huu kuendelea kujadiliwa na Diaspora wa Tanzania Duniani.”
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Na HARID MKALI
mkali@live.co.uk.
27/04/2022.
UWEKEZAJI KATIKA ARDHI USIO NA TAHADHARI, UNAWEZA KURUDISHA UKOLONI WA KIARABU ZANZIBAR.

Kuna masuala kadhaa ya kuyazingatia kuhusu Zanzibar na umiliki wa ardhi. Kabla ya Mapinduzi, Zanzibar kulikuwa na aina mbili za ukoloni: ukoloni wa kiingereza na ukoloni wa kiaarabu. Na hii ni kweli ya kihistoria.
a) Kabla ya Mapinduzi ya Januari 1964, ilikuwa ni marufuku mtu mweusi kumiliki ardhi Zanzibar.
b) Serikali ya Mapinduzi ilileta mgao wa haki wa ardhi usio na ubaguzi.
c) Tanzania Bara inayo ardhi ya kuweza kuwa-“absorb” ndugu zetu wote wa Zanzibar bila matatizo. Ndiyo sababu Kikatiba wanaruhusiwa kumiliki kiasi chochote cha ardhi Bara; ingawa watu wa Bara hawarusiwi kumiliki ardhi Visiwani.
“The United Republic of Tanzania has enough land to go around for the time being.”
d) Lakini hawa wamatumbi waliopewa ardhi na Mapinduzi wakiruhusiwa kuuza hiyo ardhi kiholela, na kwa kuwa wana kwa kuhamia ikibidi, basi wale ndugu zetu waliokimbia pamoja na Sultan Jamshid Januari 12, 1964 wanaweza kurudi na kununua kila kipande cha ardhi huko Visiwani kwa mgongo wa Uwekezaji – kwani visenti vya mafuta vipo huko Oman.
d) Tusipoangalia, kufumba na kufumbua, tunaweza kujikuta watu weusi watakaobaki huko Visiwani ni watumishi wa ndani – na nchi inaweza kujikuta imegeuka kuwa ni “Arab state of Zanzibar – literally and figuratively,” kama ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi Matakatifu ya Januari 12, 1964.
These scenarios may appear far fetched today, but they are not beyond impossibility.









