0 0
Read Time:1 Minute, 9 Second

TANZANIA IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Maonyesho ya kimataifa ya kilimo MacFrut 2022 yamemalizika Jana kwa mafanikio makubwa. Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo Pamoja ulijumuisha wizara ya kilimo na wadau wa mbalimbali ambao walifika Rimini Italy kushiriki kwenye haya Maonyesho ya kimataifa.

Wakati akiongea na Wabongo ughaibuni Media katika kuhitimisha Mh Balozi ameeleza kwa kirefu Kuhusu Changamoto Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye maonesho haya. Sambamba na kutoa maoni yake Mh.Balozi pia amewatangazia Watanzania kujiandaa kwa maonesho ya mwakani 2023 ambayo tunahitaji maandalizi makubwa zaidi.

Katika maonesho haya Mh Balozi pia alipata nafasi ya kukutana na wadau mbalimbali ambao wameonesha Nia kubwa ya kuwekeza Hasa kwenye sekta ya kilimo Cha matunda na mbogamboga.

Balozi Mahamoud Thabit Kombo katika mazungumzo na wadau wa uwekezaji
Balozi Mahamoud Thabit Kombo akiwa na Wakurugenzi wa WABONGO UGHAIBUNI MEDIA WU® , Kagutta Maulidi na Kader Alassane.
KUMALIZIKA KWA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO RIMINI ITALY, NDIO MWANZO WA MAONESHO MAPYA 2023 “Mh Balozi amewataka wadau kujiandaa mapema”
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy, Mh Mahamoud Thabit Kombo akiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mashirikiano ya Afrika Mashariki wa Uganda Mhe. Rebecca Kadagga, ambaye alishawahi pia kuwa Spika wa Bunge la Uganda , Mh Rebecca alikuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo nchini Italia “MacFrut 2022″

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %