0 0
Read Time:51 Second

WU® MediaPRODUCTION

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mh. Mahamoud Thabit Kombo ametembelea Wilaya ya Ascoli Piceno Mkoa wa Marche nchini Italia. Mh. Balozi pia amekutana na Watanzania wanaoishi katika Wilaya hiyo. Pamoja na Diaspora Balozi amekutana na Mstahiki Meya Mhe. Marco Fioravanti na Mhe. Guido Castelli ambaye ni Waziri wa Uchumi wa Mkoa huo wa Marche. Katika mazungumzo yao wamejadili mashirikiano ya karibu ya kibiashara na kiuchumi kwa kuwajumuisha WanaDiaspora na Wafanyabiashara wa Tanzania . Miongoni mwa maeneo makhsusi yaliyojadiliwa ni uwezo wa Mkoa huo wa Uzalishaji wa Mafuta ya Kula, Ngano nzima na Matunda ya aina ya Zaituni ambayo yanajulikana hapa kama Olive Ascolani, yaani Zaituni za Ascoli Piceno.

Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Uongozi wa Ascoli Piceno pamoja na Baraza lao la Wafanyabiashara kuhudhuria Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Italia na Tanzania litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 30 mwezi Septemba 2022.

Mwaliko huo ulipokelewa na Uongozi na kuthibitisha mahudhurio yao katika Jukwaa na Tamasha hilo kubwa la kibiashara.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %