0 0
Read Time:59 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Ndege ya Precision Air PW 494 iliyoanguka katika Ziwa Victoria umbali wa mita 100 kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba ilikopangwa kutua ilikuwa ikiendeshwa na Kapteni Buruhani Rubaga ambaye ni rubani mzoefu wa ndege ambaye amekuwa na shirika hilo kwa takribani miaka 20.

Afisa wa kwanza kwenye ndege hiyo ametajwa kuwa ni Peter Omondi.

Ndege hiyo, iliyopata ajali ilikuwa na watu 43

Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa, amewasili mjini Kagera muda huu.

IDADI YA WALIOFARIKI YAONGEZEKA, WAFIKIA 19:

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema mpaka sasa idadi ya waliofariki katika ajali ya Ndege ya Precision Air wamefikia 19 huku akisisitiza kuwa kwa namna ndege hiyo ilivyotumbukia katika ziwa Victoria kwa kutangulizi kichwa hakuna matumaini ya rubani wa ndege hiyo kuwa hai.

Waziri mkuu amesema hayo akiwa katika eneo la ajali baada ya kuwasili mchana wa leo na kuongeza kuwa zoezi linaloendelea na kwa sasa kinachoendelea ni utambuzi wa watu waliopoteza maisha na kufanya utaratibu wa kuwapata ndugu zao.

Wabongo Ughaibuni Media tunaungana na Watanzania wote katika kuomboleza misiba ya Ndugu zetu waliopoteza Maisha na tunawapa pole Ndugu na jamaa waliofiwa na wapendwa wao katika ajali hiyo, vilevile tunawaombea majeruhi wote Mungu awaponye. Amin.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %