0 0
Read Time:3 Minute, 22 Second

WANEC WAMSHAURI HARAKA MWENYEKITI WA CCM TAIFA KUHUSU HAYA!

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Desemba 12,2022
.

I.Haiwezekani mpaka leo ada ya Mwanachama wa CCM kwa Mwaka mzima iwe Tsh 1200/=.Yaani Dr Philip Mpango alipe 1200/= kwa Mwaka mzima!Yaani Dr Mwigulu Nchemba alipe pia 1200/= kwa Mwaka,Cde Daniel Chongolo alipe Tsh 1200/=,hii hapana haiwezekani!Yaani Mama Samia alipe ada ya Tsh 100 kwa mwezi kama ada?

Je,waajiriwa wetu ndani ya Chama maisha yao yakoje?Je,kipato chao hakiwaweki kwenye “ethical dilemma” hasa wakati wa teuzi za wabunge,madiwani na hata Chaguzi za ndani ya Chama?

II.Mchakato wa uteuzi wa makatibu Uenezi wa Chama wa Mikoa unapaswa kuwa strategic sana hasa wakati huu tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

VIJANA wa CCM karibia 10,000 mwaka 2020 tana wasomi walijitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea wa Ubunge kupitia CCM! Uchaguzi wa hivi karibuni wa ndani ya Chama katika ngazi mbalimbali pia umetupa kapu kubwa la vijana ambao nadhani wakichambuliwa vizuri na kuwapa semina elekezi wanaweza kutufaa sana kuelekea mwaka 2025!

CCM ni Chama kikubwa Afrika na ni lazima kitoke KWENYE mazoea na kwenda kwenye kufanya kazi kwa weledi kwa maana ya kuwatafuta Makatibu Uenezi wa CCM wa Mikoa wenye sifa”Qualifications,Skills, achievements” katika maeneo yao!Semina za mara kwa mara zitawajenga haraka kujua majukumu yao haraka zaidi!

Tunahitaji Makatibu Uenezi wenye sifa kuu tatu (I)Kujua dhana nzima ya Public Engagement,pili wajue ndani nje dhana ya (Ii)Political Communication na tatu lazima wawe ni (III) watu wenye kujua na kuishiba vizuri Itikadi,maono,MATAMANIO na direction ya Serikali ya awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu Hassan!Basi!

III.Jumuiya za CCM lazima ziwe active sasa kudeal moja kwa moja na matatizo ya watu katika makundi yao kwa haraka weledi na wakati!

Nataka kuona UWT kuanzia ngazi ya Taifa mpaka kule wilayani,UWT inayobeba ajenda kubwa kwa kuanzisha haraka madawati ya ya ya changamoto kubwa mbalimbali kama ukatili,ujaslimali,miradhi,Wanaume kuwatelekeza watoto na related women’s issues!UWT lazima isome Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/25 na kutambua haraka maeneo yake ya kufanyia kazi kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wa maendeleo!

Sitaki kuiona tena UWT tu ya kusimamia sikukuu za wanawake tu,sitaki kuiona UWT ya Makongamano pekee,lazima tubadilike HARAKA kumsaidia Rais kufikia malengo yake kabla ya Mwaka 2025.

VI.Nataka kuona UVCCM ile ya wakati fulani ya kina Ndugu Martin Shigella,Ndugu Nchimbi,Ndugu Anthony Mtaka,Ndugu Steven Mwakajumilo na wengine wengi!Nataka kuona UVCCM ambayo inakuwa kama Chuo cha Uongozi kwa VIJANA wa CCM na Taifa kwa ujumla.

Nataka kuona UVCCM yenye maono ya miaka 100 mbele ya hapa,UVCCM ya vijana wenye maarifa ya nini kinaendelea duniani na kuweza kutafsiri fursa za duniani kwa kuzileta katika muktadha wa NCHI yetu Tanzania!”Localisation”.
Nataka kuona UVCCM ambayo inaenda sasa kutengeneza “Think Tank” ya vijana wenye uwezo mkubwa wa kutoa majibu ya maswali magumu kuhusu maendeleo ya Taifa,nataka UVCCM ambayo itajitofautisha kwa mbali zaidi na JUMUIYA zingine za vijana ndani ya vyama vya Siasa Nchini,Afrika na huko duniani ikiwezekana!

V.Nataka kuona vijana wa CCM wenye uwezo wa kujibu hoja za wapinzani wetu kwa takwimu,utafiti na ushawishi mkubwa kwa lengo la kujenga uhalali wa kile tunachokifanya kwa watanzania!Sitaki kuona vijana wa CCM wenye Kila siku kupost picha za Mama,hii haitusaidii!
Leo Mama kaenda China,leo kaenda Dubai,leo kaenda Mtwara,kesho Mbeya!

Nataka vijana wa CCM waqualify na quantify umuhimu wa ziara za Mama nje na ndani ya Nchi kwa lengo la kuzipa uhalali kwa watanzania wote.

Tukishafika levels hizo ndani ya Mwaka mmoja ujao,CCM na Mgombea wetu wa Urais Mama Samia Suluhu Hassan,Wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani watakuwa na kazi rahisi sana 2025.

Mwandishi ni kijana-kada wa CCM, Makamu wa Rais wa zamani, Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani Idara ya Habari-Maelezo, Ofisa Kadeti wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi wa zamani Chuo cha Saut na Tumaini na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %