
Porojo na Ndarire Bila Ndaro za @โจAbuLuLuFaJM
Nakumbuka Zamani, Huku Mitaani Kwetu Ambako Mnapaita Uswahilini au Kwa Lugha ya Kisiku Hizi Uswazi, Kulikuwa na Tabia Moja Linapokuja Swala la Harusi au Hata Unyago.
Wengi walipendelea kuita vikundi vya ngoma na haswa ngoma ya Mdundikoโฆ Ngoma hii ilikuwa ikipigwa na kina baba na wachezaji wengi walikuwa ni kina mama na watoto wadogo.
Siku hizi ngoma hii haipo tena labda kupatikanaji wake ni wa nadra sana. Sasa hivi kuna vikundi vingine kama vile Mchiriku au Mnanda, siku hizi wanaita Singeli, kuna pia Baikoko na vinginevyo.
Ndio utakuta wengine nahisi ndio hawa wamekuwa wapiga debe wa mabasi ya daladala vituoni na wengine nadhani kama wameajiliwa kuwa mgambo wa manispaa.
Wapigaji wa ile ngoma ya Mdundiko enzi zile walikuwa kama ngwagu kwa kuzoea kwao kupigapiga zile ngoma, kiasi ambacho nahisi wakikosa kupiga basi hamu yao umalizikia kwa watu wengine na haswa kwa wake zao.
Kuna wanaume ambao mpaka leo wanadhani, kwa akili zao fupi kuwa kupiga wake zao ndio kuonyesha kuwa wao ndio wanaume wa ukweli.
Juzi kati hapa kwetu jamaa mmoja mwenye akili fupi kama hizo, ambaye daima haoni tabu kumshushia mkewe kipondo kama vile anapiga ngoma ya Mdundiko au Mganda, Siku hiyo yalimkuta makubwa maana siku hizi anatembea kama yule ndege Pengwini, huku anachechemea.
Siku hiyo hisiyo na jina, wapangaji wote tulikuwa vyumbani mwetu, baada ya kutoka kundimana kutwa. Kama mnavyojua hizi nyumba za kupanga zisizo na dari unasikia kila kitu nini mtu anafanya au anafanyiwa.
Si ajabu kwa kila chumba kusikia sauti za redio au Luninga ya stesheni tofauti. Huku wengine utawasikia wakikoroma wengine wakicheka wengine wakinungโunika, ndio maisha yetu tena ya kila siku.
Ghafla bin’vu, tukaanza kusikia vikombe na sahani zikivunjwa, kelele za mabishano makali yakaanza. Tukajua jamaa yetu kishalianzisha kwa mkewe kama ilivyo kawaida yake.
Kisa haswa kilikuwa jamaa katafuta chupi yake haioni.
Taabu ikaanza jamaa kama kawa akaanza kumshushia kipondo mkewe puuโฆ puuโฆ puh! Mama wa watu akaanza kulia kwa uchungu.
Tukaenda kuamulia ugomvi tukakuta wamejifungia ndani, ikawa sasa ni kujaribu kumsihi jamaa. Kila tulipogonga kumsihi afungue mlango, alitujibu โHayawahusu tokeniโ Tukabaki kusikia tu kilichokuwa kikiendelea kule ndani.
MUME: Shenzi weweโฆ (puuhโฆ puuhโฆ puuh!), huna akili (puuhโฆ puuhโฆ puuh!) chupi yangu iko wapi, umeshahonga kwa mabwana zako, (puuhโฆ puuhโฆ puuh!).
Ni wazi kabisa, mwanamke alikuwa anashindiliwa ngumi nzito nzito.
MKE: Uuuuuuuuuuuuhwiiiโฆ! Mume wangu unaniua bure sijui mwenyewe umeweka wapi!
MUME: Kufa (puuhโฆ puuhโฆ puuh!), kufa shenzi we (puuhโฆ puuhโฆ puuh!), Wanakufa panya itakuwa weweโฆ!
MKE: Baba watoto nisamehe kumbukua mimi mjamzito, muogope Mungu Mume wangu, acha ndekwa!
MUME: Kwanza mimba siyo yangu (puuhโฆ), Malaya mkubwa (puuhโฆ).
Ghafla kukawa kimyaaaaaaa! Mke halii wala mume haongei na ngumi zimesimama.
Tukajua mambo mawili yeshatokea aidha jamaa kamdedisha mkee au kauwa mkeweโฆ! Punde, dakika chache tukasikia sauti nyembamba ya ukali, kama mtu anayeugua ugonjwa wa pumu ya puaโฆ!
MUME: We malayโฆ ntakuuaโฆ.! Nasema ntakuuaโฆ (kisha kikapita kimya cha dakika tatu nzima).
MUME: Nakwambia niacheโฆ!
Mke kimya.
MUME: Aise! Ntakufanya kitu kibaya sana niachie nakwambia!
Mke kimyaaaโฆ
MUME: (Kwa upole, uku sauti ikitoka kama mgonjwa wa pumu) Unajua unaniumiza mwenzioโฆ!
Mke kimyaโฆ
MUME: Aise niachie bwanaโฆ!
Mke kimyaaa, tunasikia tu ile sauti ya kupumua.
MUME: Nyamtondo mke wangu pliiizi niache, naomba uniachieโฆ Unajua utaniua kizazi mke wanguโฆ niachie nakuomba. Mama mpenzi naomba niachieโฆ mwezioo, Oooh! Mmmh! iiiiihโฆ Uuuuwii, We mwanamke niachie mwenzioo, Aaakh!
Huku nje wambea tukashangaa vipi leo mkota anabembeleza? Kuna nini?
MUME: Ndugu zangu nisaidieni mke wangu ananiua ukuuu, uwiii ananiua ameshika nanihiiiuuuuโฆ Jamani nisaidieniโฆEeeeH Mmmh! iiiiihโฆ Uuuuh, nakufa mie mwenenu, iiih, aaah!
Kwa kuwa mlango ulikuwa umefungwa ilituchukua muda kuuvunja, wakati huo jamaa tumemkuta hoi bin taaban, kijasho kikimtoka sanjari na machozi, yaliyochanganyika na makamasi mepesi kama mgonjwa wa mafua, vyote vinamtoka kwa pamoja, mke katulia kimya, ameminya sehemu nyeti.
Nadhani yule mwanamke atakuwa katumia uzoefu na ujuzi wake wa kukanda unga wa chapati na maandazi. Si kwa koleo lile, ilituchukuwa wanaume sita na nusu, kumpapatuaโฆ
Yaani ilikuwa sawa na jeshi la mgambo kama si la sungusungu kukamata Ikulu na nchi ikasalimu amriโฆ!
Jamaa yetu akawa mpole kuliko mwanasesere wa kuchezeaโฆ!
Ana mwezi wa pili na siku kadhaa sasa anatembea kama wale Pengwini au Bata mzee!








