0 0
Read Time:36 Second

WAZIRI KABUDI AKUTANA NA MABALOZI WATATU:

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi leo, Jumanne Disemba Mosi, amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini akiwemo wa China, Finland na Sweden katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo Nje jijini Dar es Salaam.

Mbali na mazungumzo hayo Waziri Kabudi pia amepokea barua ya pongezi kutoka kwa Balozi wa China Nchini, Wang Ke iliyoandikwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi.

Mbali na balozi wa China, wengine waliofika kwa nyakati tofauti kuzungumza na Waziri Kabudi ni pamoja na Balozi wa Sweden Nchini, Anders Sjoberg na Balozi wa Finland Nchini, Riitta Swan.

BaloziwaChina #BaloziwaFinland #BaloziwaSweden #WangKe #AndersSjoberg #RiitaSwan #WaziriKabudi #Kimataifa

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %