0 0
Read Time:5 Minute, 0 Second

Na Kizito MpangoJALIMU

Wakati Rais wa El Salvador akinuia kutangaza kuwa biashara ya pesa za kidijitali (BITCOIN) kiwa ni biashara halali nchini humo, watu wengi duniani hawamjui mvumbuzi wa BITCOIN. Ni mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao. Sarafu moja ya Bitcoin kwa Tanzania ni sawa na shilingi 83,026,221.83/=.

BITCOIN ni zao la utundu wa wataalamu wa kompyuta (Programmers). Dunia ya leo matumizi ya kompyuta ni kama “haki za binadamu” tu! Hayakwepeki kabisa. Lakini ni nani hasa alivumbua BITCOIN?

Kwa kiasi kikubwa mvumbuzi anaweza kuwa MTU au KIKUNDI CJA WATU ambacho hakijulikani. Ni kama hapa kwetu Tanzania kwa uwepo wa mtu anayejiita KIGOGO ambaye ni msumbufu wa vichwa vya watu. Kila sekta yupo, “unmoved mover.” KIGOGO kama binadamu wengine wakati mwingine anatoka kapa! Katika BITCOIN jina linalobebwa zaidi ni SATOSHI NAKAMOTO.

Jina la SATOSHI NAKAMOTO ni kama KIGOGO tu kwani hakuna anayejulikana wazi kuwa ndiye mvumbuzi wa BITCOIN. Huenda wanajificha au anajificha kutokana na sheria za fedha za nchi mbalimbali kuifanya Bitcoin kuwa haramu. Watu mbalimbali wamehisiwa kuwa ndiyo SATOSHI NAKAMOTO kama vile ilivyo kwa makisio ya kuwa KIGOGO ni nani hapa kwetu Tanzania.

DORIAN SATOSHI NAKAMOTO Mmarekani mwenye asili ya Japan ni mmoja kati ya wanaohisiwa kutokana na jina lake la pili na la tatu lakini katika mahojiano alikataa. Saa tano baada ya mahojiano katika tovuti ya muhusika/wahusika wa Bitcoin iliandikwa “I am Satoshi Nakamoto.” Walijuaje kuwa kuna mahojiano yamefanyika? Bado wavumbuzi/mvumbuzi wa BITCOIN anajipambanua kwa jina la SATOSHI NAKAMOTO.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %