
Na Dr Yahya Msangi
TOGO -West Afrika
Kwanza nikiri binafsi sioni tofauti kubwa baina ya bajeti toka awamu ya kwanza.
Vyanzo vya mapato almost vile vile, matumizi kupangiwa zaidi ya maendeleo n.k. Mwenye ushahidi kuwa kuna awamu ilikuwa na vyanzo vipya na maendeleo kupangiwa fungu kubwa zaidi ya matumizi auweke hadharani tuuone.
Na toka awamu ya kwanza hakuna bajeti ilitoa nafuu tofauti. Mwenye ushahidi auweke mezani.
Bajeti hii haina tofauti na ya miaka iliyopita. Wanaodai inaumiza ni Kweli lakini bajeti ya mwaka you haikuumiza watu?
Ni matumaini yangu huko mbele serikali iitishe kikao na wadau kujadili vyanzo vipya vya mapato. Imeanza vizuri kwenye simu lakini kuna vyanzo kibao bado havijaguswa.
Mfano kuna nchi zinatoza kodi ya taka! Najua wachumi uchwara (bush economists) wataona ajabu! India na Brazil ni nchi zinakusanya fedha kibao kutokana na kodi ya taka. Na kodi ya taka imechochea kujengwa viwanda vya kuchakata taka na kutoa mamilioni ya ajira.
Kuna kodi ya vipodozi baadhi ya nchi na imeingiza mapato kibao. Umewahi kujiuliza kwa nini kila kona kuna vipodozi vinauzwa? Hapa hâta wamama wanaolaumu watakawia macho! Ndio Ufilipino vipodozi vinaingiza pato kuubwa kwa serikali. Unawatiza wanaoana kujichubua kuwapa nafuu wanaotaka mchèle washibe na watoto.
La pili ni huu mjadala naouona mitandaoni. Watu kulalamika na kuacha kushiriki bajeti inapoandaliwa. Huenda Elimu kwa umma haijakaa Sawa au uzembe tu.
Kwenye kuandaa bajeti au mswada Sheria inaagiza pawe ushirikishi jamii kupitia “Public Hearing”. Mkiti mhusika wa kamati ya bunge anaita wadau Karimjee Hall au Dodoma. Mazoea ni vikao Kati ya 2-3. Kama kweli unaguswa na mswada, bajeti ya wizara au bajeti kuu ya serikali unaenda kwenye Public Hearing kwa gharama zako. Mbona akija Olomide unalipa 100,000 kukata mauno? Mbona wakija Kaizer unalipa halafu na mnatolewa? Kwenye Public Hearing huna habari unakuja kujifanya mchumi Facebook! Ikiwa huwezi kuhudhuria Karimjee au Dodoma unatuma barua pepe kwa Mkiti kamati husika ya Bunge.
Haya yote hukufanya unaanza kuchambua bajeti mitandaoni!
Watanzania haswaa vijana ni vyema mjue kuna public hearing. Unaweza kushiriki. Usichoweza kushiriki ni kujadili ukishaletwa bungeni. Inakuwa kazi ya wabunge. Lakini unaweza kwenda bungeni kuwatongoza baadhi ya wabunge kuwa hapa ni hivi, pale ni vile! Enzi zetu tulikuwa na orodha ya wabunge rafiki kwenye masuala yetu ya ajira. Kina Misanga, Khadija Ngozi, Mustafa Nkulo, Sébastien Kinyondo, na wenzao. Tunawaita chemba. Ukumbuni wanaongea! Ilikuwa Waziri WA kazi akituona eneo la bunge anajua tumefuata nini! Waulize kina Chiligati na Kapuya!
Hâta kama ulichopendekeza kimeachwa hapo ndio una haki ya kuhoji. Lakini hii wenzio wakishiriki public hearing wee uko busy kutoga masikio, kusema umbeya, kusafisha kucha, kucheza singeli n.k. halafu bajeti ikitoka unajifanya unajua sanaaaaa ni……