George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 20,2021.
Najiuliza kwanini Uteuzi wa madc umekuwa ni ajenda kubwa kwa vijana?sio mtaani sio mitandaoni kwa sasa ajenda ni Uteuzi wa Mama!Sitaki kuamini kuwa madc ni wakubwa kuliko marc!Swali langu ni “why” mjadala umekuwa mkubwa kwa madc na wala haikuwa hivyo kwa Marc?why?
Watia Nia wa CCM hasa wa ubunge mwaka 2020 ndio kama wamepigwa na butwaa,sijui kwanini wamepigwa na butwaa,sijui kwanini wanaweweseka?sijui walikuwa wanawaza nini?jamani watu zaidi ya 10000+ na wakati nafasi za madc labda ni 150+.Hapa mnalaumu nini?
Kwa haraka haraka,almost asilimia 70 ya madc wamerudi wale wale na hapo ndio tunapaswa Kuanzia mjadala huu!Je wamefanya vizuri sana?je kuna kitu mamlaka ya Uteuzi imekiona kwao? “promosing future”,kipimo kilikuwa nini?,je walio mtaani wengi hawana vigezo?je tuna tatizo katika kutafuta watu sahihi na kuwaleta kwa platform?
Jana kabla ya mkeka kutoka nilikuwa nimekaa kaka yangu sehemu,nikawa namuuliza,”….hivi kaka yangu hawakuoni?,mbona mimi nakuona kwamba unaweza ukaisaidia Tanzania?,nikaenda mbali zaidi kwa kumuuliza,”mbona haustahili kuwa hapa?…”.Unapomuona Kaka yangu eti mifumo ya utambuzi haimuoni basi ujue pana tatizo sehemu tena kubwa.
Baada ya nusu saa ya maongezi yetu,nikamwona Kaka yangu huyu anainuka,anashangilia,nikamuuliza Kaka vipi?”…umeona mkeka wa mama…..?”nikastuka kidogo!Nilidhani anashangilia kwamba yumo kwa mkeka kumbe alikuwa anashangilia “kupigwa chini” kwa dc mmoja hapa Mbeya.Nikastuka zaidi,nikataka kujua why anashangilia kupigwa chini kwa huyu DC!
Mpaka tunaachana saa sita usiku sikuwahi kujua why alishangilia!Na hapo ndio nataka kuanzia kuuliza maswali machache juu ya Uteuzi huu kwa niaba ya sisi wa mitaani!Watu huku mitaani wanauliza maswali haya;
KITAA WANASEMAJE KUHUSU MKEKA WA JANA?
1.Mbona wale vijana wa CCM kwa jina maarufu watia nia zaidi ya makada 10000+ hawajaonekana kwa mkeka?,je,hawakuwa na sifa,hawana uzoefu,hawana elimu?Kaka yangu mmoja,mtia nia amenipigia simu asubuhi anakasema….”Kaka umeona mkeka?,hata wewe…..?,nikachekaa”.
2.Ndugu yangu Ole Mushi amekuja na andiko zito Baada ya Uteuzi wa jana na alikuja na maswali ya msingi sana na moja ya hoja yake ilikuwa kwamba tatizo letu vijana wa CCM tumeaminishwa tukisifia ndio tutapata teuzi kumbe tunakosea.Mushi anasema,kuchaguliwa kwa vijana wengi wa cdm kwenye mkeka wa mama sio kwa bahati mbaya bali kuna sababu za msingi!
Ndugu yangu Ole Mushi anataka kusema vijana wale zaidi ya 10000+ Watia nia wa Dkt Bashiru walikuwa watu wa mapambio tu hawana akili kumkichwa!Dah.
3.Wanafunzi wangu wa pale Tumaini University wawili wamo ndani ya mkeka wa mama!Nakajiuliza hivi nao wamo?nawajua uwezo wao na ukomo wao!Hivi nani na ni “machinery” zipi zinazoleta watu hawa kiasi kwamba Kaka yangu niliyekuwa nae Jana hazimwoni?
4.Mbona huku mtaani kwangu”mawilayani” naona hakuna mabadiliko ya kiasi hicho kiasi kwamba sioni “justification” ya wateule wengi kurudi?Pale kwangu Kyela pamechoka sana lakini mkuu wangu wa pale naona kapewa nafasi kwingine!Hakuna watu wa kutusaidia zaidi ya hawa?hivi kipimo cha kuwa dc mzuri ni kipi?
Hivi dc anapimwa kwa kipi?tulimpa malengo yapi?je wametimiza?
5.Uteuzi wa makada wa juu kabisa wa uvccm kwa maana ya Mwenyekiti na Katibu unatupa fundisho gani?Je,Mama anataka kujenga uvccm mpya?,Mama anataka kusema jamaa wale wamefanya vizuri sana?,Mama anataka kusema nini kwetu vijana?kuna swali zito sana kwa sisi vijana wa CCM na lazima tulijibu.
Nakubaliana na Kaka yangu Thadeo Ole Mushi kuwa vijana wa CCM lazima sasa TUJIANDAE kuja na hoja nzito la sivyo tutaendelea kuitwa mataga kila SIKU!Nimechoka kuitwa Mataga mie!
Kazi Iendelee!
+255784159968.