0 0
Read Time:1 Minute, 43 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 22,2021.

Uwepo wa kelele za hapa na pale kuhusu teuzi zinazoendelea hasa hizi Uteuzi wa madc katika Taifa umenifanya nijifikilishe kidogo kwa ajili ya kuipa afya akili yangu!Mara nyingi sisi Wakufunzi Vyuoni chakula yetu kikuu ni “thoughts” kwa maana ya fikra na bila kufikiri basi unaweza kupata tabu sana darasani.

Kuna mambo makubwa matatu nataka niyaweke kwenye muktadha hapa leo kwa lengo la kuangalia dhana nzima ya vyama vya siasa na Uteuzi unaoendelea!Nianze hivi!

NINI MAANA YA CHAMA CHA SIASA?

Kwa tafsiri isiyo rasmi sana”…..Chama Cha siasa ni kikundi cha watu chenye lengo kuu moja la kuitafuta dola na baadae kuitawala…”.

Kikundi hiki cha watu ndio tunakiita Wanachama wa Chama cha Siasa na Wanachama hawa mara zote wanatambulika kwa sifa maalumu za kichama zilizokubaliwa kwenye Chama husika(muda wa Uwanachama,Maadili yao,Kanuni zao na kadhalika).

Lazima watu hawa wawe na imani moja ya Chama husika na waweze kuitetea imani hiyo kwa gharama yoyote ile,na hicho ndio Chama cha siasa.

DHANA YA KUITAFUTA DOLA NA KUIKAMATA!

Dola kwa maana ya Serikali utafutwa kwa mbinu za kila aina kwa maana ya jasho na damu wakati mwingine!Kwahiyo dola utafutwa na Wanachama kindakindaki wa Chama husika kwa “gharama” kubwa na mwisho ikipatikana wanachama wa Chama husika ujiandaa kuitawala!

NINI MAANA YA KUTAWALA DOLA?

Kwa tafsiri isiyo rasmi kutawala Dola ni kushika madaraka ambapo makada wa Chama husika uunda Serikali yao kupitia kutekeleza Ilani husika ya chama husika!Rais kwa niaba ya Chama chake uteua Wanachama wenzake katika nafasi mbalimbali kwa lengo ya kuunda Serikali yake.Kwahiyo katika mtazamo wa kutafuta Dola na kutawala,lazima watawala Dola watokane na Chama kilichoitafuta Dola.

JE,NI LAZIMA WALIOITAFUTA DOLA WAITAWALE DOLA HUSIKA?

Nataka watalaam wa mambo ya siasa waje hapa watupe elimu kuhusu swala husika kwani kwa uelewa wangu Rais ana mamlaka ya kuunda Serikali yake na mtu yoyote anayeona anamfaa!

Mwisho wa siku wote tunaijenga Tanzania kwahiyo nina mnukuu Mh Rais Samia Hassan aliposema….”…tutamchukua Mtanzania yoyote ambaye tutaona atakuwa na mchango kwa Taifa….”.

Kazi Iendelee!

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %