0 0
Read Time:4 Minute, 45 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 22,2021.

Juzi nimemsikia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Tulia Ackson Mwansasu akishauri kuwa umri wa kustaafu kwa Wahadhiri katika Vyuo vikuu vyetu uende zaidi ya miaka 65 kwani bado wanakuwa na nguvu za ubobezi zaidi.

Nikajiuliza maswali kidogo kwamba miaka 65 huyu Mzee kweli atakuwa na nguvu za kusoma “scripts” za wanafunzi mia saba na zote akazipitia kwa umakini ule na kutoa alama kwenye mitihani kwa haki?

Ni wazi kuwa ongezeko la vyuo vikuu Nchini miaka ya 2000 halikuendana na kuwaandaa wakufunzi wenye sifa hasa katika vyuo vikuu binafsi kiasi kwamba kuna baadhi ya wakufunzi kwenye baadhi ya vyuo vikuu vyetu walikosa sifa zinaambatanishwa na TCU kwa mtu kuwa Mhadhiri.

Mpaka muda huu tunaongea kuna uhaba mkubwa wa Wahadhiri hasa katika ngazi ya Wahadhiri waandamizi angalau wenye kiwango cha udaktari wa Falsafa na Maprofesa kiasi kwamba vyuo vikuu binafsi zimekuwa vikiajiri Maprofesa wastaafu kutoka vyuo vikuu vya Umma wakati vyuo vikuu vya Umma navyo havizalishi Wahadhiri wa kutosha kutokana na kutokuwepo kwa “intensive succession plan” kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kigezo cha GPA na uhaba wa fedha katika taasisi husika!

SABABU ZA KUKOSA WAHADHIRI KATIKA VYUO VIKUU VINGI NCHINI KWA SASA!

1.Bado nifumo yetu ya elimu na mifumo ya kuwapata Wahadhiri imekaa kikoloni sana kwani mpaka leo hii Mwanafunzi bora wa kubakizwa kuwa Mhadhiri imebaki kuwa suala la ukubwa GPA badala ya kuangalia “knowleged based approach”.,!Una nini kichwani na sio una nini kwenye makaratasi yao kwa maana ya cheti.

Mfano,kuna watu wana GPA kubwa lakini hawana muendelezo wa maarifa kwa maana uwezo wa kufanya changanuzi katika maeneo yao ya masomo japo waliweza kupata GPA kubwa katika mitihani yao hivyo kufanya vyuo vikuu kuwaacha watu sahihi wa kubaki vyuoni hasa kwenye vyuo vikuu vya Umma!kwa mfano kigezo cha Mhadhiri Msaidizi kuwa angalau na GPA ya 3.8 katika ngazi ya shahada ya kwanza na GPA ya 4.0 katika shahada ya pili ni cha kizamani sana!Je,tumuache Mwanafunzi mwenye maarifa makubwa kwa sababu ya kukosa GPA ya 3.8?Kama ana GPA ya 3.7?!Hii rigidness inatupoza kila siku.

Kwanini kigezo cha “interviews na uwingi wa maarifa ya Nje ya GPA kisitumike kuwapata watu wazuri?sometime tunakosa watu wazuri wa kubaki vyuoni kwa kigezo cha GPA tu mfano mtu unamwacha kisa ana GPA ya 3.7 badala ya 3.8 na mara nyingi unakuta mtu huyu yupo competent zaidi ya mwenye GPA kubwa.

TCU mwaka 2018 wamefukuzwa walimu wenye uzoefu wa miaka kumi kwenye Kufundisha kisa mwalimu huyu ana GPA ya 3.8 ya Masters badala ya GPA ya 4.0.Yaani Unataka kusema miaka kumi aliyofundisha mtu huyu haiwezi kufidia hizo points mbili za kufikisha GPA ya 4.0?Huu ni umangimeza wa kiwango cha juu kabisa na ndio unafanya leo kusiwepo na Wahadhiri hasa katika vyuo vikuu binafsi!Rejea TCU walichofanya kwenye kampusi nyingi za Saut Mwaka 2018.

Kama tumeweza kubadilisha mifumo kwa kuwaruhusu watu kama Erick Kishigo kutopitia mifumo yetu ya kawaida na akaweza kwenda Chuo kikuu na mwishowe akaweza kupata daraja la kwanza”first class”, kwanini kwenye suala la uhadhiri tunaendelea kung’ang’ania ma GPA badala ya competence na experience ya mtu?tunakwama wapi?Tunakwama wapi?

2.Kutokuwepo kwa motisha ya mishahara mizuri na stahiki zingine kumepunguza sana morali ya vijana kosomea au kutaka kuwa Wahadhiri katika vyuo vikuu vyetu na hivyo kufanya idadi ya Wahadhiri kuendelea kupungua!Kama mpaka sasa Mhadhiri mwenye ngazi ya Shahada ya pili kwenye vyuo vikuu vingi binafsi analipwa “Take home 1.4M unategemea nini wakati kijana wenye shahada moja pale TCRA analipwa mamilioni ya fedha unategemea nini?

Nani atakuwa tayari akae darasani kwa maana ya kuitafuta shahada ya pili kwa maana ya vyuo vikuu kwa maana ya miaka mitano alafu ukaja kumlipa 1.4M tu hapo bado hajakopa Banki,bado mafuta ya gari,bado nyuma ya kupanga!Kwanini vyuo vikuu visiwe na uhaba wa Wahadhiri hasa vya binafsi?Mbona tunacheza na elimu yetu ya juu jamani?

3.Uwepo wa wimbi kubwa la Wahadhiri kukimbilia siasa kutokana na uwepo wa maslahi makubwa kwenye siasa pia kuneongeza pengo kubwa la kukosa Wahadhiri vyuoni hasa katika sekta ya Umma!

Wakati Mh.Mbunge mwenye elimu ya darasa la saba mpaka la kumi na mbili angalau anakunja mpaka Tsh 10M wewe unataka kumlipa Mhadhiri wa Chuo Kikuu mwenye shahada ya pili TSh 1.4M jamani, mbona hatuna aibu kabisa!

Kwanini tunacheza na mambo ya msingi katika uhai wa Taifa jamani!Kwanini tunashindwa kuwa serious angalau kidogo tu kwa hawa watu?

Wakati Naibu Spika Dkt Tulia anafikilia solution hii ya muda mfupi sisi kama Taifa tunapaswa kuanza kufikilia solution pana ya elimu yetu kuanzia mifumo ya kutolea maarifa,aina ya wakufunzi ambao tunapaswa kuwa nao vyuoni!Naweza kusema tuna Wahadhiri wepesi sana katika vyuo vingi kutokana na mifumo yetu mibovu ya kuamini katika GPA.

GPA kilipaswa kiwe kigezo kidogo tu cha kuwafanya watu wawe Wahadhiri vyuoni kwani tunaacha watu makini wengi Mitaani sababu ya kukosa point moja au mbili ya GPA zetu lakini watu hao wana uwezo na uzoefu mkubwa katika sekta zao za ubobezi!

Kwanini uzoefu mfano, wa miaka kumi kazini usingetumika kucomplement mapungufu ya mtu ambaye labda hata GPA ya 3.7 badala ya 3.8 ambayo inatakiwa pale udsm lakini mtu huyu kashapata uzoefu kazini wa miaka zaidi ya kumi?Mmekazana kuangalia GPA na sio uzoefu wa kazi matokeo yake tunakuwa na waalimu na Wahadhiri ambao ni totally ni theoretical based kwani hawajawahi hata kufika field kama wao mfano katika sekta ya habari!

Vyuo vikuu vyetu vianze kutoka haraka kwenye minyororo hii ya utumwa kwani tunafanya mambo ya karne ya ishirini wakati huu ni karne ya 21.TCU badilikeni kwa heshima ya elimu ya Tanzania.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %