0 0
Read Time:5 Minute, 31 Second

Jicho la Uledi lamuona Mh David Mwakiposa Kihenzile!

George Michael Uledi.
Tabora,Tanzania.
June 23,2021

Naweza nikasema mchakato wa ndani wa CCM wa kuchakata watia nia wa Ubunge mwaka 2020 ulikuwa bora sana pengine kuliko michakato mingi ya nyuma na pongezi za pekee ziende kwa Chama cha Mapinduzi na Serikali yake chini ya hayati JPM,Makamu wake wa Rais wa wakati hu Mh.Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM wa wakati huo Ndugu Bashiru Ally Kakurwa.

Kuna kitu cha kujifunza kwao kwamba kwanini michakato ya CCM ya wakati ule iliweza kuibua watu makini zaidi wenye “potential”kubwa kama ambavyo mwenyekiti wa CCM wa wakati huo hayati JPM aliwahi kusema”…..nahitaji watu wenye potential…”.

Moja ya hazina na Mashine ambayo iliweza kuibuliwa na mchakato ule ni Kijana wa miaka 37 kwa sasa Mbunge wa Mufindi Kusini David Mwakiposa Kihenzile!

KWANINI NASEMA HAYA KWA KIJANA HUYU?

1.Katika umri wake wa miaka sio zaidi ya 36 ameweza kuteka “shoo” kubwa katika jamii hivyo kuonekana ni Kijana ambaye ni hazina kubwa kwa CCM na Taifa kwa ujumla!Katika umri wake wa miaka 37 alishapata nafasi ya kuwa DAS wa Jjij la Arushakwa kuaminiwa mapema na mamlaka za Uteuzi.Kumbuka pia kijana huyu pia ni Rais wa Redcross Tanzania kwa sasa!
Kwa mujibu wa waliowahi mwandika kwenye Mitandao ya kijamii ndiye rais wa Redcross mdogo kuliko wote duniani na rais TRCS wa kwanza mdogo zaidi kutokea Tanzania tangu Redcross ianzishwe Nchini mwaka 1962.

  1. Pamoja na misuko suko kadha wa kadha lakini, Katika umri wake wa miaka 37 aliweza kupenya kwenye kura za maoni kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo lake na kuwa mteule wa CCM jimboni Mufindi kusini na kupata ushindi wa kishindo wa 98% kwa mwaka 2020 na kuingia Bungeni kwa mara ya kwanza 2020.

3.Akiwa anashiriki Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya kwanza kama Mbunge aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara na Mazingira huku Kamati hiyo ikiwa na Wabunge wakongwe na haikuwa kitu cha kawaida sana kwa Kijana wa umri wa miaka 37 kufanya haya katika Tanzania.

4.Baada ya kuweza kufanya makubwa na kuonyesha Uongozi wa matokeo katika Kamati ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kwa muda mfupi na kuweza kuaminiwa kama Mwenyekiti wa Kamati husika aliweza kuchaguliwa tena na Bunge nzima kuwa miongoni mwa Wenyeviti watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiti hiki cha Mwenyekiti wa Bunge hakijawahi kukaliwa na Kijana wa aina yake kwa maana ya umri tokea Uhuru wa Tanzania,kumbuka kiti hiki kilikuwa “special” kwa Wabunge wakongwe kama Mzee Andrew Chenge na Mzee Idd Zungu kwani angewezaje kukalia kiti hiki Kijana wa umri wake?,anaingia Bungeni kwa mara ya kwanza kumbuka!Huyu anaingia kwenye vitabu vya historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

5.Baada ya kuendesha mjadala wa kwanza wa Bunge kama Mwenyekiti wa Bunge ndipo mimi nilipoanza kuitafuta historia zaidi yake kwani aliendesha kwa weledi na utulivu wa hali ya juu mjadala ule.Pongezi kubwa kwa CCM kwa kutengeneza vijana wa aina hii!

MIFUMO YETU ITUSAIDIE KUWAIBUA VIJANA WENGI KAMA HAWA KWA MASLAHI YA TAIFA KWANI WAPO WENGI!

Nilipofwatilia Kijana huyu David Kihenzile Mwakiposa nilikuja kugundua kuwa ni mtu ambaye tayari ameshaweza kuweka alama zake katika maeneo yote aliyopita na ndio maana anakuja kwa kasi ya ajabu!

Katika umri wa miaka 37 alishawahi kuwa mtandaji wa Kata kama sijakosea ya Ubungo na kufanya makubwa katika kata yake.Ni Kijana ambaye kila unapompa nafasi anakupa matokeo makubwa!

Nenda Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania”Tanzania Redcross Society” uone aliyoyafanya katika kipindi cha Uongozi wake kama Rais wa Redcross Tanzania! Jamno ambalo hadi leo limevutia wengi kutamani kujiunga na zaidi wengi kutaka kiwa sehen ya uongozi wake kuanzia Wilaya Mikoa hadi Taifa.!

Natamani kuona mifumo yetu ya utambuzi unawaleta vijana wengi wa aina ya David Kihenzile katika “Platform” za utumishi katika Taifa kwani wapo wengi na wanaweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwa haraka zaidi!

Teuzi zinazoendelea katika Taifa kwa sasa zimethibitisha kuwa Chama cha Mapinduzi na Taifa kwa jumla kuwa lina hazina kubwa ya vijana wenye uwezo wa kusukuma Tanzania kwa haraka zaidi ni suala la kuwapa nafasi tuu!

Wakati anagombea mwaka jana niliwahi andika juu yake nikitabiri makubwa kwake ambayo sehemu kubwa yameweza kutimia hata kabla ya mwaka mmoja haujaisha katika utumishi wake.

Nilipojaribu kufuatilia kwa walio karibu, aliosoma naye na aliofanya kazi nao nikabaini mambo makubwa matatu ambayo nimeona niweze kuyaandikia ili vijana wengine waweze kujifunza toka kwake.

1) Unyenyekevu na utii. Pamoja na uwezo mkubwa aliona nao Mh David Kihenzile,karibu wote wanaomfahamu wanamwelezea kama “…ni kijana mnyenyekevu na mtii, “Hajimwambafy” wala kudharau wengine, ana heshimu walio juu yake,walio chini hata walio kwenye level moja,ni kiongozi ambaye ukiwa juu yake utafurahi maana hatataka kujiona yeye anajua zaidi ya Mkuu wake lakini pia ukiwa chini yake….”,Mmoja wa watu wa karibu wanasema.

2) Maono na Mipango, nilizungumza na baadhi ya Viongozi kutoka Jijini Arusha alikofanya kazi pamoja na wale wa Redcross na wengi wanakiri “…..David ni Mtu mwenye maono na hajali kuhusu kuchelewa,Yuko tayari hata kufanya jambo leo leo ambalo matunda yake atavuna baada ya miaka 10, Hili ni funzo kubwa kwa vijana kwamba wasiwe na haraka”. David alikuwa Mtendaji Kata,hakujali udogo wa nafasi hiyo bali aliendelea kuifanyia kazi huku akijipanga kwa mambo makubwa mengine. “..Ukimsikiliza jinsi anavyo argue kuhusu matatizo ya Nchi na suluhu yake unaridhika kuwa CCM ina utajiri ya hazina…..”.

3) Ucha Mungu, wakati vijana wengi hukata tamaa mapema, David ni kijana wa tofauti. Pale ambapo jambo lake halikufanikiwa hasiti kumtaja Mungu. Utamskia mara kadhaa akisema “Tusubiri wakati wa Mungu”. Hii ni kete muhimu sana katika Uongozi wa kisasa.

4) Mh David Kihenzile inasemekana pia sio kiongozi anayeamini kwenye Kiki. Sio mtu anayefanya kazi ili kuonekana.Katika majukumu yake ni mara chache kuona anaambatana na vyombo vya habari kwa Nia ya kutafuta Political maleage. Yeye anafanya kazi na media zinamkuta kazini. Aina hii ya viongozi tunawahitaji sana katika Taifa kwa sasa!

5) Elimu na Maarifa. Ukimsikiliza Mh.David Kihenzile “anaargue” kwa takwimu zenye usahihi mkubwa usahihi.Kila akisimama kuzungumza jukwani hutakosa kutaja takwimu.Ni kijana anayejua anachoongea haongei kwa uzoefu pekee. Aidha ni muumini wa elimu ndio maana pamoja na Kuwa na Shahada lukuki bado anaifukuzia Shahada ya Uzamivu yaani (PhD).

Kuna kitu kikubwa cha kujifunza kwa vijana wengi katika Taifa toka kwake!Vijana lazima tudrive ajenda kubwa wakati huu wa Mama Samia kwani kaonyesha wazi kwamba anataka kututumia.

Mwandishi ni Kijana na Mkufunzi wa zamani Vyuo Vikuu vya Tumaini na Saut,Ofisa Habari wa Serikali- Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %