0 0
Read Time:4 Minute, 37 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 25,2021.

Kuna kosa tunafanya kubwa kama Taifa kwa sasa na kosa lenyewe lipo katika kutaka kuvifanya vyombo vyetu vya kikakatiba kama mahakama,takukuru,Bunge na hata Polisi kuonekana kuwa ni vyombo vinavyokosa weledi kwa kiasi hiki katika kutekeleza majukumu yake.

Maamuzi kinzani yanayoendelea kwa sasa ndani ya vyombo husika kwa kubatirisha maamuzi yao wenyewe ya hapo nyuma sio tu kwamba yanaweza kuwakosesha Wananchi imani kwa vyombo vyao mbeleni bali yanaweza kuua kabisa kuaminika na kuheshimika kwa vyombo husika kwa jamii na wasaka haki.” Lacking ligitimacy”.

Juzi nimesoma mahali kuwa Ndugu yangu Tundu Lissu anapaswa kulipwa kila ambacho hakutendewa haki na hasa kwa Bunge,Leo nimesikia mahakama pia imeamua kubatirisha hukumu yake yenyewe dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema na wenzake na kuitaka Serikali kurudisha zaidi ya Tsh 300+ milioni zilizotozwa kwa wafuasi wa Chadema huku Poti wangu Mwakitalu “DPP” nae anaendelea na zoezi la kuchomoa watu magerezani na mahakamani kila siku.
Sio kitu kibaya kama kweli tumejiridhisha kwamba haki haikutendeka kwao!Ni mwanzo mzuri kabisa wa kupongezwa.

Wakati Mama yangu na Rais wangu Mh. Samia Hassan anaangaika kuweka Taifa sawa kwa kile kinachoitwa kutibu vidonda kwa lengo la kuliweka Taifa pamoja, jamaa zangu wa Chadema wameshaanzisha “Katiba Mpya Movement”,yaani daktari anakutibu kidonda huku unaanza kurukaruka na kumpigia kelele!Wasiwasi wangu Mama na Rais wangu Samia ataziweza kelele za hawa jamaa huku vijana wa CCM kwa sasa ni kama kauoga ka kukabiliana na vijana CDM kanaanza kuwaingia,they are at stand still yaaani!Hawajui wakae kimya au wamlinde Mama?

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %