0 0
Read Time:5 Minute, 14 Second

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya!
June 26, 2021.

Saa zingine ni muhimu kujiuliza maswali magumu kwamba Je, Tanzania tuna ndoto ya kuwa Taifa kubwa angalau kwa Afrika tu? kama jibu ni ndio, je, tunafikaje huko?, nani atatupeleka kwenye ndoto ya kuwa Taifa kubwa angalau katika Bara la Afrika?

Hivi tunaweza kuwa Taifa kubwa kiuchumi kama mpaka leo Taifa lina mawazo ya diplomasia ya kiuchumi ya aina moja ya kuvutia uwekezaji “FDI’s”? Hivi kwa nini hatuwazi kutoka nje ya mipaka yetu na kwenda kuwekeza kama kweli tunataka kuwa Taifa kubwa barani Afrika na baadae duniani?

Utajiri wa leo wa Ulaya kila mtu anajua ulipatikana kupitia uporaji katika mabara mengine na mpaka sasa Ulaya inaendelea kupora utajiri wa Afrika kupitia dhana mpya ya uwekezaji (Ubepari Mamboleo) “Neo-Imperialism”. Nani katwambia Waafrika kwamba tunaweza kuendelea kwa kupitia kutanua uwanja wa uwekezaji wa nje “FDI”?Ndio tunaweza kuendelea lakini maendeleo hayo yatakuwa so temporary!.

Kama kweli tunataka kuwa” The African Superpower” lazima diplomasia yetu ya kiuchumi ianze kuwaza tofauti “two ways flow” kwa maana ya kuvutia wawekezaji kuja ndani lakini pia kupeleka mitaji yetu kama Taifa nje kwenye mataifa dhaifu.

Hili ndio jukumu moja kubwa la idara yetu kwamba ina hakikisha tunayatambua mataifa dhaifu kisera na sheria na kutumia fursa hiyo kushauri Taifa kwenda kunyonya uchumi wao na kueneza mila zetu katika mataifa dhaifu.

Huwa najiuliza, hivi tunashindwaje kama Taifa kutumia madhaifu ya majirani zetu kutanua maslahi yetu?Hivi inakuwaje tunashindwa kwenda kutafuta maslahi yetu Congo ambako mataifa ya Ulaya yamekuwa yakinufaika na utajiri huo sisi tumekaa kimya! Je, ubalozi wetu wa Congo unafanya nini nje ya kulinda maslahi yetu ya kiusalama?maslahi yetu ya kiuchumi yanapatikanaje Congo?

Viongozi wangu wa CCM wana ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa? kama wana ndoto hiyo kweli, tunafikaje? kwa ramani ipi na lini?

CHINA NA MRADI WAO WA KUITAWALA DUNIA KIUCHUMI NA KIUSALAMA.

China Belt & Road Initiative ni mpango mkakati kabambe wa Chama cha Ukomunisti cha China uliobuniwa chini ya gwiji wa siasa Uchumi wa China XI Jinping Rais wa Jamhuri ya watu wa China mwaka 2014.

Nanukuu maneno haya “China’s Belt & Road Initiative forges intertwining economic, political and security ties between Africa and China, advancing Beijing’s geopolitical interests…”.

Huu ni mpango wa Taifa la China kwenda kutafuta maslahi ya China nje ya mipaka na hii ndio njia pekee ya kuitawala dunia kiuchumi, kiusalama na kisiasa, hii ndio maana ya kuwa Taifa kubwa duniani!

Huu ni mpango wa kuifanya China kuwa “Centre”, hivyo kutawala biashara ya dunia kupitia aridhini, majini na angani. Mpango huo unatekezwa kupitia njia kuu mbili, na hivyo kuweza kuzifanya nchi lengwa “targeted” kuwa mateka wa China na kuweza kunyonya Utajiri wa dunia.

Mpango maono huo wa China umegawanywa katika maeneo makuu mawili yaani “Silk Road Economic Belt” na “Maritime Silk Road” ambao una lengo la kuiunganisha China kupitia mnyororo wa Bandari kutoka kusini mwa dunia kwenda Afrika ili kuweza kuvuna Utajiri wa Afrika kupitia “uwekezaji”.

MRADI WA BANDARI YA BAGAMOYO NI MCHORO WA RAMANI YA KUVUNA UTAJIRI WA AFRIKA MASHARIKI NA KUSINI.

Uwekezaji wa China barani Afrika mpaka kufikia mwaka 2014 ulikuwa umezidi uwekezaji wa Nchi ya Marekani huku nchi tano za Afrika zenye uwekezaji mkubwa kutoka China ni Angola, Congo, Ethiopia,Afrika Kusini na Mauritius.

Mpango huo wa China wa “Maritime Silk Road”, unataka kuifanya Tanzania kuwa lango la kunyonya utajiri wa Nchi za Afrika ya kati ,mashariki na kusini pia hasa katika Nchi ya Zambia ambako Uchina imekuwa na njaa ya kuvuna shaba yote ya Zambia kupitia uwekezaji.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo una malengo makuu matatu kwa Nchi ya Jamhuri ya watu wa China;

  1. Kurahisisha kuvuna utajiri wa madini katika Nchi za Zambia na Congo na kuweza kuyasafirisha kutoka Zambia na Congo kwenda Nchini China kupitia Bandari ya Bagamoyo bila bugudha!

Hii ina maana kwamba madini yote ya shaba na makaa ya mawe yaliyokuwa yanapitia bandari ya Dar es salaam kutoka Zambia yataenda kupitia Bandari ya Bagamoyo.

  1. Kutokana na uwezaji mkubwa unaotarajiwa katika mradi wa Bandari ya Bagamoyo, wafanyabiashara wengi kama sio wote watalazimika kukimbilia Bandari ya Bagamoyo na kuiacha Bandari ya Dar es salaam ikifa kifo cha kujitakia.

Ni wazi kuwa uwekezaji wote uliofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika sekta ya Bandari “Tanga, Dar es salaam na Mtwara utakuwa hauna maana kwani utashindwa kurudisha gharama za uwekezaji husika “returns on investment” kwa sababu Bandari ya Bagamoyo obviously itavutia zaidi wafanyabiashara kutokana na ufanisi wake.

3.Mradi wa Bandari ya Bagamoyo inaenda kuuwa kabisa Bandari ya Mombasa na kuzifanya Nchi za Afrika mashariki kuwa tegemezi. Kwa mfano, Mradi wa SGR ya Kenya ambao ulilenga kuhudumia Bandari ya Mombasa pia unaenda kufa.

Ni wazi gharama za kupitishia mizigo katika Bandari ya Bagamoyo huenda zikawa za chini kabisa ili kuweza kuuwa soko la Bandari za Dar es salaam,Tanga,Mtwara,Lamu na Mombasa.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unaenda kuuwa “foward & Backward link” tuliyokuwa tunataka kuitengeneza kama Taifa kwa maana ya “link” ya Bandari ya Dar es salaam na SGR yetu ili kuweza kuongeza mapato ya Serikali.

Kuruhusu ujenzi wa mradi Bandari ya Bagamoyo ni kuhatarisha usalama wetu kama Taifa na kama jumuiya ya Afrika Mashariki. Hata kama Bandari ya Bagamoyo haitogharimu senti yoyote bado haina faida kwa maslahi mapana ya kiulinzi ya Taifa letu.

Usalama wa Nchi ni bora zaidi kuliko vipande kumi vya fedha tutakayoenda kuipata! Sisi ni Taifa la mfano katika kulinda maslahi ya Afrika kamwe tusiwe sehemu ya kuubeba mpango huu wa China.

Kwanini vitu vya kimkakati na vyema maslahi ya Usalama kwa Taifa hatuwazi kuvifanya wenyewe kama Taifa?Tuna Tatizo gani?Uwekezaji wowote wa majini lazima utazamwe kwa jicho la kiusalama zaidi kuliko kiuchumi zaidi!

Otherwise labda kama mradi wa Bandari ya Bagamoyo tuutekeleze wenyewe kama Taifa kwa fedha zetu za ndani labda hapo Watanzania watawaelewa!Kwani tunaweza kukosa hizo Tsh Trilioni 23 za kutekeleza mradi huo?Hata kama tutautekeleza kwa miaka 15 ni bora zaidi kuliko kuutekeleza na Uchina kwani uchina ana mahesabu makali zaidi katika mradi huo na lazima atatuzidi akili!

Nawasalim katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Acha kazi Iendelee!

Mwandishi ni kada na kijana wa CCM,Mkufunzi wa zamani vyuo vya Saut na Tumaini,Ofisa Habari wa zamani,Idara ya Habari Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha na Mtia Nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %