
Jicho la Uledi
George Michael Uledi!
Kyela,Mbeya.
June 28,2021.
Leo Rais alikutana na wahariri wa vyombo vya habari Nchini Ikulu Dar es salaam na kuwapa nafasi ya kumuuliza Mh Rais maswali kwa niaba ya Watanzania.
Sijutegemea kabisa kwamba kati ya WAANDISHI zaidi ya kumi waliopata nafasi ya kumuuliza Mh Rais maswali hakuna hata mwandishi mmoja aliyeuliza swali kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo ambao ndio mjadala mkubwa zaidi unaoendelea katika mitandao ya kijamii na Mitaani kwetu!
Kwangu mimi pamoja na Watanzania wengi,swala la mradi huu wa Bagamoyo lilikuwa muhimu sana kwa Mh Rais kuulizwa ili kupunguza sintofahamu pia kutuliza mijadala na taarifa potofu zinazoendelea.Mradi wa karibia Tsh Trilioni 23 alafu mmekaa kimya?tuna shida gani wanahabari?
Nataka tuwaze pamoja,Je wahariri hawa je leo wametenda haki kwa Watanzania?
Mnataka Mama Samia awape nini?awaulizie maswali?Kwa kweli mmetuangusha sana na njie ndio mnafanya mjadala huu uendelee wakati tungeweza kupata majibu mazuri kutoka kwake na hivyo kupoza joto ya mjadala huu ambao wengine wamekuwa wakiupotosha!

+255784159968.








