0 0
Read Time:4 Minute, 58 Second

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
June 29,2021.

Chama cha Mapinduzi tayari kilishaanza mipango mikakati ya kuitafuta Ikulu mwaka 2025 kupitia mipango mbalimbali ya wazi na mipango ya kificho na kwa weledi mkubwa!Ni kawaida kuona kila kitu chao CCM kinakuwa kinaratibiwa kwa umakini mkubwa mfano,angalia kesho wapo kwenye kikao chao pale Dodoma chini wa Mwenyekiti wao Rais Samia Suluhu Hassan!CCM mara zote wanatembea katika mpango vita wao kwa umakini mkubwa.

Ndugu zangu wa Chadema baada ya kutoka kwenye “jela ya siasa” ni kama hawajui wapi wanapaswa kuanzia kwani kwa sasa inaonekana ni kama kila kitu wanataka wapewe kutoka kwa mamlaka!Ni kama mfungwa anapotoka gerezani na kuja mtaani kwake kila kitu kilichopo mtaani anakitaka yeye na mfungwa huyu asipoangalia anaweza akajikuta anavunja Sheria na kurudi tena jela alikotoka!Uhuru wa manyani unaitwa!

Ni wazi kuwa uwanja wa vita vya siasa Nchini umebadilika sana,kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa sio muda mdogo hivyo Chadema baada ya kutoka katika kifungo cha kisiasa walipaswa kutokurupuka kwa kiasi hiki na kuanza kutaka kila kitu wanachohisi walichokipoteza kwa mara moja,haiwezekani sana!utulivu wa kimkakati ni muhimu sana katika siasa!

RAMANI YA CHADEMA KWA SASA ILIPASWA KUCHORWA HIVI!

1.Kitengo cha utafiti wa sera na Usalama cha Chadema sijui kama wanajua kinachotakiwa kufanywa kwa Sasa! Nadhani kilichopaswa kufanywa ni kufanya utafiti wa hali ya siasa Nchini kwa sasa kwa kuanza kuikagua CCM ya sasa,Serikali ya sasa na mwisho kumkagua Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujua dhamira,maono na dira yake!Achana maneno ya majukwaani,kitengo cha Usalama cha Chadema kilipaswa kwenda mbali zaidi kujua masuala ya msingi ndani ya CCM.

Ujasusi huo “political intelligence” ungewasaidia kujua ubora na udhaifu,na ubora wa Serikali ya awamu ya sita hivyo mipango yako”political strategy” yao ingeanzia hapo kwanza na sio kukurupuka na ajenda ya “Katiba mpya”kwa sasa!Mh Rais Samia Hassan leo ametangaza wazi wazi kuwa suala la Katiba sio kipaumbele kwa sasa!Msimamo huu wa Rais na CCM ulipaswa uwe umejulikana na majasusi wa Chadema mapema kabisa,otherwise kama wana ajenda nje ya siasa kuhusu mpango huo.

2.Chama makini hakiwezi kubeba ajenda za mwaka 2010 wakati wa JK na kuzileta mezani leo bila kujua na kumkagua Mwenyekiti wa CCM na Mh. Rais kujua ni yapi maslahi yake na kipaumbele chake kwa sasa!Huu ni udhaifu mkubwa sana katika siasa za kisasa!

Chadema wao walishajiaminisha kirahisi sana kuwa Mh. Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan angeweza kufungua kila mlango kwa ajili yao kwa lengo la kuleta umoja wa kitaifa,haya ni makosa makubwa!Hakukuwa na haja ya kuanzisha “Katiba Mpya Movement ” kwa sasa na huko ndio kukurupuka na kukosa umakini kwa chama cha siasa makini kinachowinda Dola.

3.Utafiti kwa maana ya “Political Intelligence auditing”ungeweza kuwaambia tuanze na kipi kwa sasa na kwa maoni yangu,wakati huu ulikuwa ni wakati wa kuweka sawa maswala ya Uhuru wa kujieleza,Uhuru wa kufanya siasa pamoja na Uhuru wa vyombo vya habari kwani hizo ndio “platform” kuu za kufanya siasa safi katika Taifa kwa wapinzani hasa kipindi hiki ambacho milango ya kufanya siasa ilikuwa imefungwa.

Kwenda kuanzisha madai ya Katiba mpya kwa sasa wakati huu ambao mambo yao mengi bado hayajakaa sawa ni kukosa kuwa “strategic” na kukosa mpango kazi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2025.

4.Wakumbuke kuwa Katiba hii”mbovu” ndio iliwapa wabunge wengi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka 2015 na kuwa ni Chama chenye ushawishi mkubwa kwa Umma kwa wakati huo!Chadema wangeanza kufanya siasa kwanza na kupitia “platform” hizo na baadae kidogo wangeweza kuja na ajenda ya Katiba mpya kwa mafanikio makubwa kuliko ilivyo kwa sasa!Ajenda ya Katiba mpya ni kama imeshafungwa kwa sasa!Ajenda hii ilipaswa kusubiliwa mpaka siku ambayo Rais atakutana nayo!Hakika ingebeba uzito zaidi lakini sio kwa sasa!

Kudai Katiba wakati huu ni kukosa “timing” kwani huko mtaani kila mtanzania anakiri kuwa Mama Samia “anaupiga mwingi” alafu wewe unataka kudai katiba,utapata wapi wafuasi?Makosa makubwa!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %