0 0
Read Time:4 Minute, 11 Second

Sensei Fundi Rumadha Godan (5 Dan)

Takriban sasa yapata miaka 700 tokea Sanaa ya mapambano ya kichina kutambulishwa katika visiwa vya Okinawa, Ryukyu, kabla ya visiwa hivyo kuwa sehemu ya Japan ya bara mwaka 1400-1500.
Hatimaye mwezi Oktoba, tarehe 25, 1936 master wa Karate kadha walikutana katika mji wa Naha ( Naha-shi), Okinawa wakiwemo majina maarfu kama vile, Hanishiro Chomo 1869-1945; Chotoku Kyan 1870-1945; Miyagi Chojun 1888-1969 na Kiyoda Juhatsu 1886-1967; Chibana Chosin 1885-1969; na Shipan Shiromo 1890-1954, na kulikubali kutumia jina la neno “KARATE” au mikono mitupu katika Sanaa za mitindo ya mapambano, ambayo leo hii ndio tunaifahamu kama Karate.
Hii ndio sababu au kielelezo kikubwa leo hii kuwa Oktoba 25 kila mwaka kuwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya Karate duniani. Sherehe hii hufanyika kati Kati ya moyo wa mji wa Naha, katika mtaa maarufu wa “Kokusai Dori” au (Mtaa wa kimataifa), kwa kuwakusanya wana wa karate mitindo yote ya Karate Okinawa, na kufanya kata mtaa mzima zaidi ya maili au kilomita kadhaa na maelfu ya washiriki toka mitindo mbalimbali ya Karate inayowakilisha dunia nzima

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %