
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 20,2021.

Rais ndio mtu pekee anayebeba maono halisi ya watu na nchi yake”vision” na maono mara zote uendeshwa na misingi mikubwa mitatu ambayo Rais au Kiongozi wa Nchi hapaswi kuionea aibu kuisimamia na misingi hiyo ni;
1.Uthubutu katika kutekeleza maono magumu hata kama kutakuwa na kelele katika Taifa kwani hakuna jinsi ya kuyafikia maendeleo ya haraka na maendeleo ya kweli wakati huo huo Rais unataka kuwafurahisha watu wengi”popular leadership”.
2.Maono ya Taifa lazima yaendeshwe na dhana nzima ya “selection and maintainance of the National aim” kwa maana ya kwamba Taifa kupitia Rais wake ukaa na timu yake na kuchagua “course of action” ya kuichukua kwa wakati fulani bila kuionea aibu na kupitia hivyo maendeleo ya watu katika Taifa upatikana!
3.Maono mazito ya Taifa pia yana gharama kubwa kwa maaana ya “pain”.Ni lazima Rais akubaliane na Ukweli kuwa kuna kipindi utalazumika kuumiza watu kwa ajili ya maendeleo yao otherwise kama Kiongozi hana uhakika na anachokifanya anaweza kuogopa kelele!Kiongozi lazima aelewe kuwa kuna kipindi cha kupigiwa makofi na kuna kipindi cha kusutwa na wale unawaongoza lakini “on the way” unaweza kupigiwa makofi kwa maamuzi yako magumu uliyochukua.









