0 0
Read Time:3 Minute, 1 Second

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
July 19,2021.

Kuna kitu labda hatufanyi vizuri katika mchakato wa kumilikisha na matumizi ya silaha kwa Watanzania hivyo kutoa nafasi ya mambo mengi ya kiharifu kuendelea kutokea Nchini kwa sasa!

Vyombo husika vinapaswa kuchukua hatua za haraka kwa kufanya analysis ya haraka ili kuzuia matukio haya kwa sasa!Mwaka jana mtu mmoja wilayani Mbeya alimfyatulia Kijana mmoja bastola na kuweza kumuua baada ya kuzuka kwa ubishi katika eneo husika mkoani hapa!

Labda mazingira ya tukio la juzi maeneo ya sinza mkoani Dar es salaam ndio labda yamesikitisha sana baada ya mtu mmoja kumfyatulia mwenzio risasi kwa makusudi na kisha na yeye kuamua kujiua wakiwa katika bar moja jijini!

KUNA MAHALI NAONA KUNA UDHAIFU MKUBWA NA PANATAKIWA KUFANYIWA KAZI HARAKA!

1.Nadhani kuna udhaifu mkubwa katika kutambua historia na tabia za watu ambazo ni hatarishi kwa umiliki wa silaha hivyo kuweza kuhatarisha usalama mtaani!

Mi nadhani kuna umuhimu wa kutafuta taarifa za ndani na nyuma ya mtu husika kabla hajapewa silaha!Mfano,kuna mtu aliwahi kupewa silaha wakati tunajua ni mtu ambaye amewahi kupoteza kumbukumbu baada ya huko nyuma kuwahi kupata ajali mbaya hivyo akili yake kutokuwa sawa.

2.Lakini pia naona kuna madhaifu katika kufwatilia tabia za watu tunaowapa silaha baada ya kuwakabidhi silaha husika!Ukifwatilia watu wengi wanaofanya matukio ya mauaji,mara nyingi uwa na historia ya kutishia watu mitaani!

3.Pia inaonekana, Wananchi wengi hawana elimu kuhusu “management” ya silaha!Watu wanapaswa wangepewa elimu ya kujua wapi anapaswa kwenda na silaha na maeneo gani mmiliki wa silaha hapaswi kwenda silaha yake!

Maeneo hatarishi kwa mmiliki wa silaha ni maeneo yenye mikusanyiko kama Bar,kwenye usafiri wa Umma,kanisani,sehemu za fukwe na kadhalika!Lakini pia watu wanapaswa wapewe elimu ya kutoa taarifa pale wanapoona mtu anatishia kutumia silaha yake katika maeneo tajwa hapo juu!

Hauitaji kubishana na mtu mwenye silaha zaidi ya kuondoka sehemu ya tukio pale unapotokea ubishana na kutoa taarifa Polisi kwa ajili ya hatua zaidi!Ni hatari kubishana na mtu mwenye silaha awe Polisi au Raia Popote unapokutana nae!

4.Wananchi lazima wajue kuwa matukio ya watu kukosa afya ya akili yapo mengi ambayo yanaletwa na mambo mengi ya msongo wa mawazo katika maisha ya kila siku!Mfano,Askari mmoja Nchini Kenya,Catherine Mungogo aliweza kuwaua wanaume wawili katika matukio tofauti na baada ya siku tisa kukutwa na yeye amejiua bafuni nyumbani kwao!

NINI POLISI NA VYOMBO VINGINE VINATAKIWA KUFANYIKA KWA SASA?

Polisi wanapaswa kuwekeza katika elimu kwa Wananchi ya jinsi ya kukaa na watu wenye silaha au wanapokutana na watu au kuhisi mtu fulani ana silaha kwa wakati husika!Ni hatari kubishana na mtu mwenye silaha kwahiyo Lazima Wananchi wawaepuke watu wa aina hiyo hasa wanapokuwa na silaha!

2.Pili,suala la Polisi kufwatilia nyendo za watu wote wanamiliki silaha ni muhimu na wakijiridhisha kwamba nyendo zao sio za kawaida wapokonye silaha hizo!Sijui ni watu wangapi wanapokonywa silaha kwa kusikia tu nyendo zao,mfano kutisha watu!

Watu wengi wananyanganywa silaha zao baada ya tayari kufanya matukio ya kutisha mitaani mfano,mauaji!Hii sio salama sana!

Kwa mtu aliyeiju silaha haswa na kweli anajua madhara ya silaha kamwe hatokimbilia kutaka kumiliki salaha!

3.Umiliki wa silaha unamwitaji mtu awe na akili timamu,anayejua maadili ya silaha lakini zaidi awe sio limbukeni wa kuwa na silaha!Wengi bahati mbaya wenye silaha mitaani hasa vijana wanakuwa nazo kwa lengo la kujimwambafy na sio kwa sababu za ulinzi wao binafsi!

Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais zamani,Daruso- IJMC ,Mhadhiri Msaidizi wa zamani Vyuo Vikuu,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha na Mtia nia Ubunge Jimbo la kyela mwaka 2020.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %