
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 8,2021.
Wanasiasa wetu hasa Chama changu tawala chama cha mapinduzi, tunapaswa kuwa na maono makubwa na kuona jinsi gani chombo nyeti kama JWTZ kinaweza kikatufanyia kazi za ziara zaidi ya zile za kawaida za Jeshi “Traditional Military Duties” na moja ya majukumu hayo ni jinsi gani chombo hiki kinaweza kuzitumia fursa katika mataifa ambako kinapewa majukumu ya kiulinzi na kiusalama kufaidisha Nchi yetu Tanzania zaidi ya sasa!
Kila siku nawaza je,Tanzania Nchi yangu, tumeitumiaje na tunaitumiaje heshima yetu ya diplomasia ya ulinzi nje ya mipaka ili kuweza kufanya Nchi hii iwe tajiri?Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache afrika ambazo Askari na maofisa wake wanaaminika zaidi kwa kuwa weledi wakati wakitekeleza majukumu yao nje ya mipaka ya Tanzania.
Fursa na sifa hii pekee ingeweza kutupa fursa nyingine ya kuwa na military istallations katika maeneo husika hivyo Taifa kupata fedha nyingi za kigeni kupitia shughuli hizi za kijeshi kwa kushirikiana na raia nje na ndani ya mipaka yetu!
Taasisi na mashirika yaliyo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yamebeba imani kubwa ndani ya Nchi kwa kutekeleza miradi mingi ya kusaidia raia ikiwemo miradi ya Ujenzi,Kilimo,ulinzi,Kuzuia majanga na kadhaa wa kadhaa hivyo,Shirika kama SUMA JKT linahitaji kupewa nguvu kidogo tu ya kuweza kuvuka na kufanya kazi zake nje ya mipaka katika maeneo yenye uhitaji wa kazi zao za ulinzi,Ujenzi,Kilimo na kadhalika!
Shirika la Nyumbu Kibaha hivyo hivyo lingeweza kutanuka na kutumia fursa zilizopo katika maeneo fulani fulani dhaifu ambayo labda yangehitaji bidhaa zake na huduma nyinginezo!
JWTZ WANAPASWA WAFANYEJE KWA SASA?
1.Kitengo cha masoko cha Suma JKT kupitia waambata wa kijeshi wangeweza kutambua haraka maeneo nje ya mipaka yetu yenye mahitaji maalum!Mfano,maeneo mengi ya Nchi ya Congo kutokana na athari za vita,miundombinu yake imeharibiwa na hata makampuni mengi ya ndani yamesitisha huduma zao za ujenzi kutokana na vita!
Je,Makampuni kama Suma JKT, wasingeweza kufika maeneo haya na kuchuma fedha kwa ajili ya Taifa kwa kuendesha miradi mbalimbali kwa kutumia diplomasia yetu nzuri na kazi ambazo JWTZ imeshazifanya za kiulinzi mfano katika maeneo ya Goma,DRC.
Ujenzi au ukarabati wa shule,hospitali,Nyumba na miradi mengine ingeweza kutupa fedha zaidi na kuongeza pato la Taifa.
2.JWTZ ina vijana kwa maana ya Askari na Maofisa wengi wenye weledi na maono makubwa kupitia kozi zao za kijeshi na kozi za kiraia,je,kwanini wasianze kuwaza kuandika miradi ya kuleta fedha hasa wale wanatoka wenye “mission” ambao wanakuwa wameona fursa nyingi zaidi.
Mfano,Vijana wa kitanzania Mainjinia wa barabara,Madaktari na kada nyingine wanakosa ajira miaka nenda rudi,wangeweza kumezwa na miradi hii ya Nje ya Nchi!Mimi naamini hakuna kinachoshindikana hapa!JWTZ Philosopy lazima ibadilike sasa kwa ajili ya kulinda maslahi na Ulinzi na Usalama wa Taifa kupitia dhana uchumi!
- Waambata wa Jeshi pamoja na kuwa na majukumu ya kiulinzi na Usalama nje ya mipaka yetu,Serikali ingeweza kuwapa majukumu mengine nje ya yale “traditional military duties” kwa kutusaidia kuonyesha fursa nje ya mifumo ya kiulinzi lakini jeshi kupitia makampuni yake yaliyopo ndani na mapya linapaswa lifikilie kufanya hivyo!
Mfano,Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kupitia Shirika lake la Nyumbu lingeweza kupata soko kubwa la magari yake hasa magari ya huduma ya Zimamoto katika maeneo ya Nchi za jirani kama Malawi,Zambia,Congo na Burundi!
Wangapi wanajua kuwa Shirika la JWTZ la Nyumbu kama sijakosea, wanatengeneza magari ya Zimamoto ambayo yanaweza kutembea katika Nchi kavu na baharuni!?Gari ili za Zimamoto uweza kufanya shughuli zake za kuzima moto likiwa katika bahari,mito mikubwa na hata maziwa!Je,Nchi ngapi zina huduma hii?Je,Nchi zilizo ndani ya visiwa haviitaji Kweli huduma hii?Tungeweza kupata fedha nyingi kama Taifa kupitia mipango kama hii!

WENZETU DUNIANI WANAFANYA HAYA!
Idara ya Ulinzi ya Nchi ya Marekani”DoD”, uendesha vituo vya namna hii”military Istallations” ndani ya majimbo ya Marekani na kuweza kutengeneza fedha nyingi zaidi kwa kuhusika moja kwa moja na ujenzi wa barabara,madaraja,shule,hospitali hivyo kuweza kutengeneza ajira kwa watu wake!
Kwa mujibu wa Ofisi ya Economic Adjustment ya DoD,gawio la Ofisi hii kwenda kwa Serikali ya Marekani wakati mwingine ufikia mpaka asilimia 7 ya GDP ya Marekani.