
Dr Yahya Msangi
TOGO WEST AFRICA
Makala zilieopita nilielewa mbinu mbalimbali wanazotumia magaidi kujipatia fedha – utekaji, wizi kwenye mabenki, wizi wa vitu vya kale, kuomba michango kwa njia za mtandao, kupitia biashara haramu na halali, kupitia NGOs zao au za wengine, kupitia charity organization zao au za wengine, n.k.
Kazi nyingine kubwa wakishapata hela ni kuhakikisha vyombo vya ki usalama haviwezi kutambua ni hela zao haswa wanapotaka kuzitumia au kuzituma.
Magaidi wanaajiri wataalamu magwiji ili kufanikisha hili. Kazi hii ya kufunika fedha kitaalamu inaitwa LAYERING. Kugubika hela. Lengo kuu ni kuziingiza fedha zilizopatikana kwenye mifumo halali ya fedha. Ndio utasikia ‘kutakatisha fedha’. Kuna wahalifu wengi zaidi ya magaidi nao hutaka kutakatisha fedha walizozipata. Mfano matapeli, wazungu wa unga, n.k. Pia ukumbuke kuna uhalifu ambao unafanyika na hela inatakasika automatically. Moja ya uhalifu huu ni kupitia dini. Unachangiwa hela kwa kuhadaa watu lakini hela hiyi automatically inakuwa kwenye mfumo rasmi wa fedha. Biashara hii haramu imevutia watu wengi haswa barani Afrika. Haihitaji mtaji mkubwa kuianzisha na mamlaka hazihoji uhalali wa utajiri wa mhusika kwa kuwa anahesabika hajaiba! Japo kujipatia fedha kwa hadaa ni kosa la jinai.
Kuna mbinu mbalimbali za kusafisha fedha (layering)
- Miamala: kupitia miamala magaidi na wahalifu huweza kuingiza fedha kwenye mfumo halali. Moja ya kampuni kubwa ya mwamala duniani ni HAWALA. Imetumika sana kutakasa fedha. Lakini miamala kama ya kampuni za simu nayo inatumika. Serikali nyingi duniani hupata shida na hizi kampuni za miamala.
- Wire Transfer – fedha kutumwa ki electronic. Mfano unataka kulipia king’amuzi unatuma kupitia simu unafunguliwa kin’gamuzi. Magaidi yanaweza kuunda kampuni ya ving’amuzi na kutuma fedha kwenye hiyo kampuni. Inakuwa ni wateja wanalipia king’amuzi kumbe hela haramu zinasafishwa. Hapa ndio wako kina M-PESA na wenzao. Mnaweza kufurahia lakini kumbe wafaidika wa kubwa ni magaidi na wahalifu na sio nyie!
- Kutumia watu wengi kutuma fedha. Wakishapata fedha wanazigawa kwa watu wao nchini na wao huanza kutuma kwa wengine ambao wako sehemu kuna hitajio la fedha. Labda wako nchi ambayo wanataka kununua silaha au kuteka mtu n.k.
- Kutuma fedha kwa watu katika nchi mbalimbali – mfano walio Tanzania wanazituma Canada, wa canada wanazituma Germany, wa Germany wanazituma Yemen, n.k. Zinazunguka nchi ambazo kuna hitaji za fedha. Kila nchi inakata kiasi kinachohitajika kilichobaki wanatuma mbele.
- Kutoa invoice bandia haswa kwenye mizigo bandarini na airport. Invoice inaweza kuonyesha makantena yana mitumba kumbe yamejaa maburungutu tupu ya hela! Kwenye bandari ambazo sio makontena yote yanakuwa scanned au walipopachika mtu wao pesa inaweza kupita kama maji!
- Kuanzisha mlolongo wa makampuni – SHELF COMPANIES, OFF – SHORE COMPANIES, SHELL COMPANIES, FRONT COMPANIES: hizi ni kampuni feki. Mfano watu wanakuja TZ na kampuni yao wanakwambia imesajiliwa Jamaica au UK. Kumbe iko kwenye makaratasi tu. Huu ndio mchezo waliocheza kina RICHMOND. It was a FAKE COMPANY. Mnairuhusu ifanye biashara nchini au ishike kandarasi. Mnairuhusu ihamishe ‘faida’ kwenda ‘kwao’! Kumbe inahamisha faida na fedha chafu ! Na huko mnakodhani ni kwao sio kwao!
Kuna wahalifu ambao biashara yao kubwa ni kuunda hizi shell companies halafu kuziuza kwa wahalifu wenzao. Yaani wanenda nchi mbalimbali kusajili hizi kampuni kwa kudai makao makuu yako kwingine. Wakishafanikiwa wanatafuta wateja wanaotaka kusafisha pesa. Wanawauzia haki ya kutumia kampuni zao mahali popote duniani kwa malipo. Magaidi au wahalifu wanazipenda maana zina sifa ya kuwa na umri mrefu toka zisajiliwe. Uwepo wao na tukio la ugaidi au uhalifu una tofauti kubwa. Huwezi kuzishuku. Hawa wanaoanzisha hizi kampuni wako tayarikujenga hata ghorofa wakijua italipa! Utashangaa kuna muda jengo linabaki bila mpangaji kwa muda mrefu. Nia sio kulipangisha bali kutoa picha kuwa kampuni ni kubwa na ya muda mrefu nchini. Ukifuatilia utaona matangazo kama ‘je unahitaji kampuni; wasiliana nasi, sisi ni wataalamu wa kuanzisha kampuni’! Unaweza hata kutumia kampuni yao kupatia mkopo! Ila utagawana nao halafu unatoweka! Benki inaambulia manyoya au kukamata jengo!
Mchezo huu unachanganya nchi ambayo masharti ya kuanzisha kampuni ni rahisi. Haswa kama hayalazilishi mwenye au wenye kampuni kujulikana kwa kina. Siku hizi kuna nchi ni mpaka uonyeshe passport ya wenye kampuni nawajue unaishi wapi.
- Kutumia brokers au mawakala nchi mbalimbali. Hela inazunguka kiasi inakuwa vigumu kwa vyombo kuifuatilia ilipo.
- Cryptocurrency: Kifedha hela za kibiashara kama dola, euro na paundi hujulikana kama FIAT CURRENCIES. Ndizo zimetumika miaka mingi kufanya biashara duniani. Sasa wataalamu wameleta CRYPTO CURRENCIES. Haijashika kasi sana lakini tayari wahalifu na magaidi wameivamia kutokana na uwezo wake wa kufichia fedha Tofauti kubwa baina ya FIAT CURRENCY na CRYPTO CURRENCY ni kwamba FIAT CURRENCY hutumia benki lakini CRYPTO CURRENCY haitumii benki. Kutumia benki kunaweka uwazi zaidi ya kutotumia benki. Kwa kuwa crypto currency inatumia mtandao njia hii inakabiliwa na udukuzi japo sio rahisi kudukua kutikana na akaunti inavyokuwa encrypted. Sawa na Whattsap na Facebook. Whattsap ni encrypted hivyo ni salama zaidi kuliko kina facebook na Twitter.
Account za crypto currency zinaitwa WALLETS (pochi). Aina kuu za crypto currency kama BITCOM na ETHERIUM zinatumia hizi pochi. Kila mteja anapewa pochi yake ambayo kwa kweli ni vigumu kuifungua kwa kuwa inatumia mlolongo mrefu wa alphabeti (Alpha Numeric Numbers). Mfano wa wallet ya mtu ni huu:
1BvBMSEYstZetqTFn5Au4m4m4GFg7xJnNVN2
Hii ni akaunti ya mtu! Kutokana na akaunti namba za aina hii inakuwa vigumu kumjua mwenye hii akaunti! Lakini kila kona ina namna yake kuikata! Sasa kuna wataalamu waliobobea kwenye fani ya CRYPTO CURRENCY na BLOCKCHAIN FORENSIC ambao kazi yao ni kuzitafiti hizi akaunti na kuwajua wamiliki. Hii ni muhimu kwa kuwa magaidi na wahalifu wamejikita humu! Wakishamtambua anayemiliki akauni ya crypto currency kinachofuata ni kumfuatilia na kuona kama amebadilisha kwenda FIAT CURRENCY ili kufanya matumizi. Ukweli ni kwamba bado dunia haijatambua CRYPTO CURRENCY kama fedha ya malipo. Mfano mwenye akaunti ya crypto currency hata kama ina mabilioni hawezi kwenda na crypto currency kununua chochote dukani au kiwandani. Itamlazimu kuibadili iwe ama Dola, ama Euro ama Paundi! Na katika kubadilisha ndio inakuwa rahisi kudakwa. Hapa ndio Lema alionyesha ujinga wake alipodai Tanzania ianze kutumia crypto currency! Ni uropokaji wa kijuha! Hajui chochote kuhusu crypoto currency. Ni wa kupuuza. Hata sasa ukiwasikia kina Mbowe wanadai crypto currency jua ni wale waleee! Nchi hazijaanza kufanya transaction kwa crypo currency. Wenye FIAT CURRENCY wamegoma! Na tayari ubaya wa crypo currency umeanza kujitokeza. Ole wake Tanzania ihadaike!
Aina kuu za crpto currency kwa sasa:
- MONERO
- DASH (Digital Cash)
- Z Cash
- BITCOM
THE END
Shukrani kwa wanafunzi wa vyuo, watumishi wa vyombo binafsi na umma na wote mliofuatilia na kuuliza maswali nje na ndani ya ukurasa huu. Itafuata: MANDELA RULES halafu NAMNA YA KUTAMBUA ANAYEKUSUMBUA MTANDAONI