0 0
Read Time:33 Second
Alphonce Felix Simbu (mwenye jaketi jeupe) baada ya kumaliza mashindano leo, akiwa na Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo Omary(mwenye jaketi jeusi), Daktari wake Juma Mwankemwa (mwenye jaketi la bluu) na mkimbiaji mwenzake Gabriel Geay (mwenye T-shirt nyeupe)

Mkimbiaji wa mbio ndefu katika mashindano ya Olympic nchini Japan anayeiwakilisha Tanzania mwaka huu Alphonce Felix Simbu ameingia katika kumi bora.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo Omary, Simbu ameshika nafasi ya SABA katika mbio za Marathoni zilizomalizika leo.

Omary amesema kwenye mashindano ya Olympic ya mwaka huu mbali na mkimbiaji Simbu, Tanzania iliwakilishwa pia wakimbiaji Gabriel Geay na Failuna Matanga ambao hawakuingia kumi bora.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %