0 0
Read Time:2 Minute, 42 Second

Na Dr Yahya Msangi

Togo West Africa

Utesaji wafungwa ulianza kitambo na uslishamiri sana enzi za vita kuu ya Kwanza na ya Pili. Ilikuwa ukitekwa (Prisoner of War – PoW) utateswa mpaka ukome. Baada ya vita kuu ya pili UN ikaamua ichukue jukumu la kulinda wafungwa. Zikatungwa kanuni (Minimum Standard Rules for Treatment of Prisoners) mwaka 1955. Zikatumika kwa takribani miaka 60. Mwaka 2015 zikafanyiwa maboresho na ndipo zikapewa jina la NELSON MANDELA RULES kwa kumbukumbu ya miaka yake 27 jela. Nchi nyingi ikiwemo Tanzania imeridhia. Ila niliwahi kumsikia yule bwana mdogo wa Ubeljiji akishitaki anakoita ‘duniani’ kwamba Tanzania inavunja NELSON MANDELA RULES! Nilicheka sanaaa! Ukweli ni kwamba NELSON MANDELA RULES sio mkataba (Convention) kwa hiyo nchi wanachama hazilazimiki kuzitekeleza! Ni muongozo tu ambao nchi mwananchama anaweza kutekeleza au kutotekeleza! Sasa kushitaki kuwa nchi haitekelezi NELSON MANDELA RULES ni ujinga mzito.

Mandela Rules zimesimama juu ya kanuni (principles) zifuatazo:

  1. Mfungwa ni biandamu na anapaswa kuhudumiwa kama binadamu (humane treatment). Kanuni hii inakataza kumtesa au kumfanyia kitendo chochote kinachodhalilisha ubinadamu wake.
  2. Kutombagua kwa sababu ya dini, jinsi, kabila, utaifa, mtizamo wake wa kisiasa, n.k. Hapa kuna mataifa yanapinga baadhi ya mambo na yamekataa kuyatekeleza. Mojawapo ni kigezo cha kutombagua kutokana na ushoga, usagaji, n.k. mataifa hasa ya kiarabu na Izrael yanadai hawa wanapaswa kubaguliwa maana kitendo chao ni cha wanyama sio cha wanadamu! Na kwa mujibu wa kanuni hii ni haki yao kukataa!
  3. Kutokatisha ujamii wake (normalization): yaani mfungwa asitengwe kiasi mahusiano yake na jamii yakazima kama kibatari. Ndio maana wanaruhusiwa kutembelewa. Nchi nyingine wanaruhisiwa waende kwao kwa siku mbili tatu wakananiii halafu warudi. Kanuni hii inataka pia kulinda haki za mume, mke au watoto wa mfungwa. Mfano afungwe mume miaka 5 mke itamwathiri. Ama mke aende au mume aende kuepusha zinaa na mambo mengineyo. Kuna nchi uarabuni mke wa mfungwa akidai uzalendo unamshinda haraka mamlaka inatoa ruksa waonane ili isihiriki zinaa!
  4. Usalama wa mfungwa au wafungwa. Mfano huwezi kuweka mtoto na mijibaba chumba kimoja mtoto akawa salama. Au ukaweka jitu lina kifua 8 pack na mwingine mnyongee kama mwanangu Ficky. Huyu mnyonge usalama wake wa kilwili na kisaikolojia utaathirika. Pia haitakiwi kwa kanuni hii wafungwa kuachwa peke yao hasa nyakati za usiku.
  5. Kurekebisha na sio kuharibu zaidi: dhumuni kubwa la kifungo ni kurekebsiha ili akirudi katika jamii asirudie au akubalike au amudu maisha. Jamii iwe salama kwa uwepo wake miongoni mwao. Ndio maana wafungwa wanapaswa kufundishwa au kusoma wakiwa jela. Nashukuru juzi kina Zitto walimpa mfungwa kitabu.

Mandela rules zinapatikana mtandaoni lakini ukitaka kusoma kozi yake jiunge na UNODC (United Nations Office for Drugs and Organized Crimes). Unasijisajili kama mdau. Acha kutoa kipaumbele kwa makundi yasiyokuongezea maarifa kama sijui SIMBA FANS! Kila saa mipasho na ubuyu! Ukiwa mwananchama wa UNODC utaweza kujiunga na course zao ambazo hulipii. Kama una NGO yako ukisoma utapata funds ufundishe maofisa magereza nchini mwako.

Nimalizie kwa kurudia: Mandela Rules ni hiyari ya nchi kutekeleza au kutotekeleza! Au kutekeleza baadhi na kuacha baadhi! Kimataifa sio kosa na huwezi kuishitaki serikali! Mwambieni jamaa wa Belgium wazungu wanacheka wakisikia anadai Tanzania imevunja sheria ya kimataifa na eti dunia iiadhibu! Atizame Guantanamo Bay wafungwa walivyotendewa! Kuna makosa ukifanya serikali inaweza kuweka Mandela Rules kando ikushughulikie. The bottom line is: haki za mfungwa zinakoma pale zinapoanzia za wasio wafungwa!

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %