

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 9,2021.
Katika siasa za dunia za vyama vingi za sasa”contemporary politics”,sio kila wakati Chama dola kinapaswa kujifungamanisha na maamuzi ya Serikali yake kwa lengo la kutunza uhalali wa kisiasa wa baadae kwa wananchi endapo mambo yatabadilika!
Mara nyingi Serikali za Afrika zimekuwa zikifanya makosa ya kisera na kimaamuzi na mfano mzuri ni Nchini Afrika Kusini ambako kumekuwa na misukosuko ya kisiasa kutokana na makosa yanayohusu maamuzi ya Serikali ya Nchi hiyo!
Kama Chama kitakuwa kinajifungamanisha na Serikali kwa kila kitu hatari yake ni kwamba endapo Serikali itaingia katika makosa basi na Chama kitakuwa kimeingia kwenye kujipaka matope yatokanayo na makosa ya Serikali!Chama makini utengeneza mazingira ya kuyakwepa matope ya Serikali ili kulinda uhalali wake kwa watu”political ligitimacy”.
Kinadharia, Mimi naamini kabisa kuwa chama “is permanent” lakini Serikali “is temporary”!CCM itakuwepo kesho na kesho kutwa lakini Serikali inaweza kubadilika!Mfano,Serikali ya awamu ya sita ya CCM imebadilika kimtazamo,uelekeo,kisera tofauti na Serikali ya awamu ya tano japo zote ni Serikali za CCM !Maana yangu ipo hapo!Kwahiyo ukuu wa Chama ni mkubwa kuliko ukuu wa Serikali kwa mantinki hiyo CCM inapaswa kuwa makini mara kumi zaidi ya Serikali yake!
DHANA KUU MBILI AMBAZO CHAMA CHA MAPINDUZI KINAPAPASWA KUCHEZA NAZO KWA UMAKINI NA USTADI MKUBWA KWA SIASA ZA KISASA!
1.Kwa bahati mbaya sana,katika Nchi nyingi za Afrika,maamuzi ya Serikali hayaanzii kwenye Chama hivyo kutokuwepo kwa dhana nzima ya maamuzi ya pamoja”collective responsibility”.Hili ni kosa kubwa katika siasa za kisasa za dunia!
Unapoona Kada kama Askofu Gwajima na PolePole wanasimama na kwenda kinyume na maamuzi ya Chama ujue hapo hapakuwa na ushirikishwaji katika maamuzi ya Serikali kupitia Chama!kosa kubwa kabisa!Kwanini pasiwepo na ushirikishwaji wakati maamuzi ya Serikali ya CCM yanawahusu Watanzania wote?
Katika masuala ya msingi kama ya maisha ya watanzania palipaswa kuwepo na kauli moja kwa wanaCCM wote lakini kwa wale ambao wangekuwa hawajakubali maamuzi hayo, kwa maslahi ya CCM, walipaswa kukaa kimya!ingetosha kabisa kutuvusha salama!
2.Lakini pia sio lazima kwamba kila wakati Chama lazima kiwe sehemu ya maamuzi ya Serikali kwani nalo ilo ni kosa la “kistratejia”.
Katika Andiko moja katika”Africa in Transition” la mwaka 2016 la Ndugu John Campbell nanukuu”….the relationship between the ANC and South African State can be ambigous,some within the ANC see the two are essentially coterminous while others, however,see the two as separate….”.
Mfano huu wa mahusiano katika ya Serikali ya Afrika Kusini na Chama chake dola yaani ANC unatupa picha ya jinsi Serikali na Chama dola CCM vinapaswa kufanya kazi!Lazima tufike sehemu tubadilike kwa maslahi ya CCM na baadae maslahi ya Taifa!
Sioni haja ya viongozi wangu wa juu wa CCM, kuwabananisha wakina Askofu na Polepole kuhusu msimamo wao kwani naona bado CCM tunaweza kuwatumia vizuri katika mipango vita yetu hasa katika “Politics of Covid -19 Prandemic” huku wakiwa na misimamo yao hiyo hiyo!Rejea nukuu ya mahusiano ya Serikali ya Afrika Kusini na Chama dola ANC.
KWANINI WATU HAWA WANAWEZA KUWA FAIDA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI PAMOJA NA KUWA NA MISIMAMO YAO!
Nawaza tu kwamba mimi ningekuwa CCM,ningejitaidi kwa nguvu zote kuunda au kuimarisha kitengo cha utafiti wa sera,matukio na mienendo ya siasa cha chama cha Mapinduzi!Hiki kitengo wajibu wake mkubwa kingekuwa kufanya “quick intervations” na kutoa taarifa kuhusu madhara au faida ya matukio,matamko na sera ambazo Chama inataka kuchukua kabla ya kuyachukua!










