0 0
Read Time:1 Minute, 18 Second

Katika pitapita yangu nimesoma ripoti hii ya Uwekezaji Duniani Mwaka 2021 yaani World Investment Report 2021 iliyotolewa na UNCTAD.

Ripoti inasema Mwaka jana 2020 katikati ya wimbi la korona bado Tanzania iliendelea kuaminiwa na hakukuwa na mabadiliko ya kiuwekezaji kutoka nje kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa majirani zetu.

Nikipitapita huku mitaani bado naona kuishinda HOFU ni silaha muhimu zaidi dhidi ya korona na nyenzo muhimu ya kuimarisha Uchumi na kuleta maendeleo kwa watu wetu.

Wakati nikipongeza jitihada nzuri za Serikali ya @ccmtanzania kuweka uchumi wetu sawa katika ya linalosemwa wimbi lingine la korona Mwaka 2021 mbinu moja tusiiache, kwamba korona si kubwa kama tunavyo ambiwa.

Yako magonjwa mengi na yanayoua zaidi, tusije tukatolewa kwenye mstari na korona, nimesoma pia wengi ya wanaoshambuliwa na korona ni wale wenye mashambulizi ya magonjwa mengine yanayoteteresha Kinga ya Mwili ambayo korona inafanya magonjwa hayo yasisemwe kwa kiwango kinachostahili.

Naomba kwa unyenyekevu kutoa rai kwamba ni muhimu sana watu wetu wakumbushwe tena na tena namna ya kujenga kinga ya Mwili ikiwemo elimu ya chakula na lishe bora kama hatua ya msingi ya kukabiliana na magonjwa na maambukizi yanayoweza kuzuiwa na kinga imara ya Mwili.

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika hili na ni Imani yangu vitatenga nafasi na kuzungumzia masuala haya kwa maslahi Mapana ya Nchi yetu, Taifa letu na Watu wetu wa Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania
Ibilisi na Huu ugonjwa wake hawana nafasi Tanzania.

NB:

  1. Kuchanja ni hiyari lakini sio kila kitu, mimi nitaimarisha Kinga ya Mwili na chanjo kwangu HAPANA
  2. Sasa baadhi yenu msihangaike na mimi, hangaikeni na rai yangu hapo juu
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %