

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
August 11,2021.
Najiuliza kuna nini kimemtokea Mwalimu wangu wa Uandishi wa Habari komredi Ernest Sungura mpaka Gazeti la Chama la Uhuru lije na “Headline” ya aina ile?,wakati asubuhi ya leo napitia Magazeti, nilistuka kidogo kuona “Headline” ya aina ile na nikadhani labda ni michezo michafu ya wenzetu kutaka kutuvuruga kumbe tulikuwa tumejivuruga wenyewe ndani ya “news room” yetu.
Lakini nikajiuliza,je, Rais Samia Suluhu Hassan kweli anaweza kutoa kauli ya aina hii kwa wakati huu?,nikasema hapana haiwezekani!Nikahisi kuna tatizo kubwa sana sehemu!wapi?,sikuweza kujua kwa asubuhi ile!
TIMU YA UHARIRI YA GAZETI LA UHURU HALIKUJUA HAYA?
Kuna udhaifu mkubwa umeonekana ndani ya chombo chetu cha chama lakini sitaki kuamini kuwa hii ni bahati mbaya au kukosa weledi!wasimamizi wakuu wa gazeti ili wote wana uzoefu sio wa kuandika tu bali pia uzoefu wa kukufunzi katika ngazi ya vyuo vikuu kama Kaka yangu Enerst Sungura na wenzake!
1.Utaratibu wa kuandaa “story” kwenye chumba cha habari uanzia mbali kidogo, kwa maana ya kwamba habari uanzia kwa mwandishi”reporter”, baadae upelekwa kwa Mhariri Msaidizi”sub editor” na baadae kwenda kwa Mhariri Mkuu”Editor”!sitaki kuamini kuwa hawa wote hawakuona au hawakujua”implication” ya story husika kwa siasa za Chama dhidi ya upinzani na kwa maslahi mapana ya Taifa!
2.Ninachojua mimi,uandaaji wa “headline” kwa maana ya kichwa cha habari cha Gazeti”Lead story” sio suala la mtu mmoja na sitaki kuamini kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyestuka baada ya kuona headline hiyo kabla ya kuchapwa!Kama Mhariri mkuu hakuona madhara ya “headline” hiyo natarajia Mkurugenzi mtendaji angestuka,kama sio yeye basi hata idara ya uchapishaji ingestuka!
3.Habari kama hii kwa Mhariri makini lazima alipaswa kujiridhisha kutoka kwa mhusika baada ya “interview” ya BBC na Mh.Rais!Rais kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu alipaswa afwatwe kabla ya “story”kwenda hewani na kuweza ku “cross check” ukweli ” Truth & accuracy” wa kauli hiyo na hapo wangepata uhakika wa kile wanalichoandika.
Kuna tatizo kubwa ndani ya Gazeti la Uhuru,sijui kama kazi “newsroom” zinafanyika kama” team” au kuna mtu anaamua anavyojua yeye!Kungekuwa na umakini,nilitarajia angalau hata “mmbeya”mmoja angeweza kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama Taifa Ndugu Chongolo kumwambia kuhusu “story”husika labda ingezuiwa mapema lakini hakuwepo “mpiga mbiu” hata mmoja!Je,ni bahati mbaya?
NINI MAANA YA HEADLINE ILE KWA UMMA?
1.Gazeti la Uhuru linajua kuwa “headline” ile ilikuwa inataka kuuambia umma kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Samia Suluhu Hassan tayari kachoka kutumikia nafasi hiyo ndani ya siku chini ya mia mbili tu kitu ambacho sio kweli!
Hii inaweza kuiweka Serikali na kuifanya isiaminike kwa Umma hivyo kukosa “public support” na hii ndio “implications” ya “story” ile!
2.Story ile inaweza kuwafanya watu ndani ya Chama kuanza kufikiria kutengeneza safu za kusaka Urais mapema hivyo kuhatarisha uhai wa Chama dola kuelekea mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.Mh Rais kasema kuwa huu ni wakati wa kujenga Nchi na sio wakati wa kufanya siasa kwahiyo kusema kuwa Rais hatogombea ifikapo mwaka 2025 ni kutaka kumfanya Mh Rais aonekane kigeugeu!Hapana na haikupaswa kuwa!
3.Kwa Gazeti la Chama kuja na “story” ile ni kuwapa wapinzani cha kusema!moja wanaweza kusema lolote lakini pili wanaweza wakadhani ndani ya ccm kuna tatizo!Kwa vyovyote vile Gazeti ili limetoa taswira hasi kwa Serikali ya awamu ya sita na Chama cha Mapinduzi na hii haivumiliki!
Uamuzi wa bodi ya Gazeti la Uhuru ni sahihi sana,uamuzi wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa ni mzuri zaidi na uamuzi wa Idara ya Habari- Maelezo ni mzuri zaidi katika kutekeleza na kusimamia weledi!
Taaluma inawaruhusu waandishi wa habari kufanya kitu kinaitwa “news analysis & news interpretation” ya kauli mbalimbali kutoka kwa “source” lakini lazima kuweka mizania ya story husika dhidi ya madhara na faida! Mara zote kauli tata huwa tunazitafutia “clarification” toka kwa “source” kwa maana ya chanzo cha habari kabla ya kwenda hewani na si vinginevyo!
Kitendo cha leo cha Gazeti la Uhuru ni kitendo ambacho kinahatarisha uhai wa CCM na Serikali yake lakini pia kinahatarisha Usalama wa Taifa kwa namna moja ama nyingine!
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Makamu Rais zamani ,Serikali ya wanafunzi Daruso -IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari- Maelezo,Ofisa Mwanafunzi za zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli,Arusha,Mhadhiri Msaidizi Vyuo Vikuu vya Tumaini Iringa & Saut na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.








