
Na H.Mkali,
London, England.
Mradi huu kama ukitekelezwa kwa mkopo kutoka nje kuna hatari ya kutokuwa na maslahi kwa Taifa letu. Njia pekee ya kuufanya mradi uwe na tija kwetu ni kuutekeleza kwa fedha zetu wenyewe siyo za mkopo. Wataalamu wa nje (wakitakiwa) waje kama vibarua wetu.
Mjadala na Wachina kama ulishindikana kuwa win – win enzi za Magufuli hauwezi kuwa win – win leo. Kutokana na ‘experience” yetu na hawa Wachina huko nyuma, wengi tuna hofu kuwa maongezi yanayoendelea yanaweza kuwa ni kuanua ngoma juani .
Aidha, haraka ya kuutekeleza huu mradi haipo kabisa. JPM ameyafanya mengi tena makubwa kuliko watangulizi wake wote. Na Benki ya Dunia ikakiri kwa kuiweka Tanzania katika uchumi wa kati. Iwapo Dr. Magufuli aliyafanya hayo bila msaada wa Bandari ya Bagamoyo, hakuna sababu ya kiongozi mwingine yoyote kushindwa kuendeleza hayo maendeleo yaliyokwisha anzishwa bila hiyo Bandari.
Kama kweli ni lazima tuendelee na hao Wachini basi makubaliano yote yawekwe mitandaoni ili wenye nchi yaani, Watanzania watoe maoni yao kabla ya kusainiwa.
Hakuna makubaliano yoyote ya kibiashara ambayo yanaweza kufanywa eti ni jambo la usalama wa Taifa hivyo iwe siri. Hayapo.
Na sisi Hatutakuwa wa kwanza kuweka mikataba mitandaoni kabla ya kusainiwa. Mama Helen Johnson Sirleaf wa Liberia alikuwa anafanya hivyo.
Mkataba tulioukataa ulikuwa unafuta uhuru wetu. Na Uhuru wa Tanzania ni mali ya Taifa – yaani mali ya Wananchi wote wa nchi yetu. Haupo mhimili ambao umepewa mamlaka ya kufuta uhuru au kuuza sehemu ya Taifa letu kwa taasisi yoyote ya nje. Mamlaka hayo hayapo popote kwenye Katiba yetu.
Hivyo basi Rais, Spika na Jaji Mkuu hawana madaraka ya kupitisha Sheria ambayo hatima yake inakuwa ni kufuta uhuru wetu na kuuza nchi; kama huu Mkataba tulioukataa ulivyokuwa.
Mama chonde, usikubali ushauri ambao utakuharibia “legacy” yako. Historia itakapokuja kuandikwa itasema wewe ndiye uliyesaini Mkataba ulioiweka nchi utumwani. Kushauriwa vibaya hakutakuja ongelea na vizazi vijavyo.

Ahsante.
mkali@live.co.uk
03/09/2021.
Muheshimiwa Raisi
Wewe na raisi mtaafu Mzee Jakaya kikwete mnamahusiano gani?
Huu mradi raisi mtaafu ndio kauleta
Baada ya kuingia babaetu mpenzi JPM aliukataa na alitoa sababu kwanini kaukataa na tukaelew
Sasa kwa nn ww umeingia2 madarakani unaurudisha huu mradi?
Muheshi ufute uwo mradi
Sion km unafaida kwa watanzania Tanzania kuna Bandar nyingi zinatosha jaribu kuangalia sekta zingine