0 0
Read Time:1 Minute, 4 Second

Na Mwandishi wetu

Taarifa zilizo tufikia katika Chumba chetu Habari zinasema kuwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italy Ndugu AbdulRahmani A. Abdallah Kosh, amepata ajali mbaya wakati akivuka barabara kuelekea nyumbani kwake , sehemu ya Luguluni karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ubungo mjini Dar Es Salaam Tanzania.
Ajali hiyo ilitokea Jana tarehe 3/9/2021 siku ya Ijumaa majira ya jioni saa kumi na moja, alipokuwa akivuka barabara kwenye kivuko Cha pundamilia na ghafla mwendesha bodaboda kama alivyotambulika akiwa katika mwendo wa kasi Sana alimgonga Mwenyekiti na wote walikimbizwa kwenye hospitali ya Mloganzila ambako bado wanaendelea kupata matibabu. Hali ya mwenyekiti Bado haijakuwa nzuri kwa mujibu wa Ndugu Allen Dastan Bendera ambaye alifika hospital yeye na mkewe Joyce Bendera mara tu walipopata taarifa Jana usiku . Kwa Taarifa za muda huu ambazo Ndugu Bendera ameeleza wakati akizungumza na studio za Wabongo ughaibuni nchi Italy, amesema majibu ya vipimo vya awali yana matumaini makubwa na yupo chini ya uangalizi mzuri wa madaktari bingwa wa Hospital ya Mloganzila. Wakati huo huo Ndugu Bendera amesema tatatibu za kisheria zinaendelea ili kumtambua aliesababisha ajali hiyo maana pikipiki hiyo imefahamika kuwa haikuwa na namba za usajili. Mwenyekiti alikuwa katika matayarisho ya kurejea nchi Italy baada ya kumaliza mapumziko yake.
Tutaendelea kuwapa taarifa kadiri tutakavyo zipata.

©2021 Wabongo Ughaibuni ®

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %