George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 20,2021.
Ni suala la muda tu ufike nishudie haya kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita, Mh Samia Suluhu Hassan.
Ni wazi kuwa huyu ni “game changer”mwingine katika Taifa kutokana na jinsi anavyowaza na kufanya mambo yake katika sura ya utofauti kabisa!Pale unapodhani Mama Samia anaenda kushoto mara zote amekuwa akifanya tofauti na wengi wanavyowaza na hii inaenda kusaidia sasa kuleta “mindset change” kuhusu jinsia na mambo mengine ya maendeleo katika Taifa.
Katika mukutadha huo,SITOSHANGAA kuona haya yakitokea kabla ya kuisha mwaka 2025 katika Tanzania;
1.Sitoshangaa siku nikisikia Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri jeshi Mkuu, kateua CDF Mwanamama pale Ngome!
Ni suala la mindset change tu kwani ni wazi kuwa CDF hatutarajii ataenda kwenye uwanja wa medani na kupigana vita!Tunahitaji sana kwa sasa CDF Mwanamama kwani wapo wengi wenye sifa ndani ya JWTZ!
Rais wa Ghana hivi karibuni,amemteua CDF Mwanamama Constance Ana Emefa Edjean- Afenu kuwa mkuu wa majeshi ya Ghana na kuandika historia mpya katika Afrika yenye mila potofu kuhusu wanawake!
2.Sitoshangaa kumuona Mama Samia Suluhu Hassan ndani ya tuzo za “Ibrahim Prize For Achivement in African Leadership”.
Infact,zile fedha za uviko -19 toka IMF japo ni mkopo, zinaweza kubadili kabisa kabisa maisha ya Watanzania ndani ya mwaka mmoja tu kama zitasimamiwa kwa dhati na wateule wake!
Utitriri huu wa wawekezaji wa nje kuja Tanzania kwa fujo, kunaweza kumpa points kibao Mama huyu kwa kuweza kutengeneza Uchumi imara na shindani ndani ya miaka yake minne ya kwanza tu!Sitoshngaa kuona akinyakua tuzo ya Mo kama sio sasa basi mwaka 2022.
3.Sitoshangaa kuona GDP ya Tanzania kufikia mwaka 2025 imeweza kufikia 100.00 USD Billion!Kuna juhudi za wazi za kukuza Uchumi wa Nchi,juzi ndege ya Shirika la ndege la Ufaransa”Air France” limeanzisha safari zake na Zanzibar tangia zikome miaka ya 1970.
Ile filamu ya kutangaza utalii ya Mama Samia,inaweza kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi tatu bora kwa kuvutia watalii katika Afrika kabla ya mwaka 2025.
Mwalimu wangu,Dkt Damas Ndumbaro unaweza kuandikwa katika vitabu vya historia ya Tanzania kwani ni wazi kuwa Kuna kazi kubwa inafanyika pale Mpingo House!
4.Sitoshangaa kuona SGR baada ya kukamilika Serikali inaruhusu sekta binafsi Kuingia katika sekta ya usafiri wa reli na hapa namuona Azam anataka kuja kuwekeza katika usafiri wa reli kwa kufanya “business deversification” toka kwenye Azam Marine mpaka kuja kwa usafiri wa reli!
Hapa namsihi ndugu yangu, Masanja Kadogosa wa TRL akune kichwa kwelikweli kuweza kushindana na wawekezaji wengine!Serikali ya CCM ya awamu ya sita tunataka kutengeneza pesa,ajira zaidi na huduma bora kwa Watanzania ili kukuza Uchumi!
Wakati Serikali imewekeza zaidi ya USD 1.5 Billion kwa mkopo wa Banki ya Standard Chartered kwa kipande ujenzi cha Dar – Makotopola tuaachaje kutafuta fedha ya kulipa deni la SGR yetu?
5.Sitoshangaa kusikia Mh Rais Samia Suluhu Hassan, ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Rais 2025 kwa zaidi ya asilimia 70.
Sitoshanga tena kusikia Wabunge wa CCM pia wameshinda kwa zaidi ya asilimia 70 ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Tulia Ackson akichaguliwa kuwa Spika mpya mwana Mama!
Sijui itakuwa vipi kwani,Rais atakuwa Mwanamama,CDF Mwanamama,Spika Mwanamama,sijui Mama ataamua kumalizia tuu kwa kumweka Mwana Mama pale kwa mhimili wa mwingine wa dola yaani Mahakama!
Wanaume mupo?Ni suala la muda tu, nadhani mpaka sasa wakina Mama”Ummy Mwalimu,Mhagama,Gwajima,MaRPC,…….” wameshaprove kwamba wanaweza kuendesha Nchi hii hata wakiwa pekee yao!
Mwandishi ni Kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha
Maofisa wa Jeshi, Monduli Arusha,Mhadhiri wa zamani,Saut -Tabora na Tumaini University Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.
+255784159968.
+255746726484.