0 0
Read Time:2 Minute, 36 Second
JICHO LA ULEDI

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 22,2021.

Ningepata nafasi siku moja ya kujumuika na wakina mama wa kitanzania ambao kila kukicha, Mh Rais ameendelea kuwapa nafasi katika Serikali yake ya awamu ya sita ningesema neno moja au mawili kwao.

1.Kwanza lazima wamama hawa “wawaprove wrong” wanaume kuwa nafasi hizi sio zawadi bali zinatokana na sifa za kielimu,sifa za uzoefu,sifa za ubunifu na mambo makubwa waliofanya huko walikotoka.

2.Maeneo waliyopewa kusimamia lazima yafanye vizuri zaidi kuliko maeneo ya wanaume ili kuwawezesha wanawake wengine kuendelea kuaminiwa zaidi!

3.Yale mambo ya msingi wanayosimamia majumbani kama walezi wakuu wa familia lazima wayatafsiri kwa kuyaleta katika mawanda ya kitaifa kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Taifa kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutimiza malengo ya Taifa,Ilani ya Uchaguzi ya CCM na malengo yao binafsi kama binadamu mwingine yoyote!

TAFSIRI YA JINSIA MWANAMKE LAZIMA IWE POSITIVE KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

1.Wakina Mama wanapoweza kutukuza bila uwepo wa baba zetu “single parent” na baadae tunakuja kushika nyazifa kubwa makazini tunaanza kuwapamba na kuwaita majina mazuri mazuri ya “Nani kama mama,mjomba ni Mama”.

Lakini, wakina Mama hao hao wanapojaribu kupambana ili waweze kuishinda minyororo ya mila potofu ndani ya jamii zao na baadae kuja kuweza kushika madaraka kazini, majina yao huwa yanabadilika na kuanza kuwaita “wanawake dhaifu na hawawezi kuongoza”.wakati wao ndio wengine waliwafikisha hapo bila uwepo wa Baba zenu.Dah,pole Mama!

2.Wakina Mama kila wanapojaribu kupambana kwa ajili ya kupigania haki zao za msingi majina yao yanaanza kubadilika na kuitwa “gender activist,wavunja ndoa na wakuda.

Lakini,Wamama hao hao wakiwa wanaangaika mahakamani kutafuta na kupambania haki za watoto wao kama matunzo ya watoto wao waliotelekezwa na Baba zao pale ustawi wa jamii na kisha watoto hao wakaweza kusoma na kukua vzr then watoto wao hasa wa kiume wanaanza kuwapamba”Nani kama mama?,Bi mdashi,Jembe….”.

3.Groupu la wakina Mama wakiwa kwenye harakati za kutafuta pesa hasa kupitia vikoba tunawaita wajasilimali,mwanamke mpambanaji na kadhalika!

Lakini wanawake zaidi ya wawili au kakikundi, wakiwa bar kwa ajili ya shughuli zao za vikao vya ujasilimali ,mnaanza kuwapachika majina”wadangaji,malaya,wauzaji…”.

Hivi Afrika nani katuroga?nani atakuja kututoa hapa?Dunia inakwenda kasi sana lakini upande wa pili wa dunia ni kama umelala!Hipo hivi;

1.Wakati Mh.Rais Samia Suluhu Hassan leo, akimteua Profesa Penina Muhando, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu huku mitandaoni Watanzania wanaume wakizusha mijadala wakishangaa kama kawaida, kule Nchini Marekani, Binti wa miaka 25 tu alikuwa anateuliwa kuwa Jaji katika historia ya Nchi ya Marekani na Taifa kubwa duniani.

2.Watati Mh .Rais Samia Suluhu Hassan akimteua Dkt Tax Sigomenda, kuwa Waziri wa Ulinzi wanaume wa kibongo wakapigwa na mshangao tena,lakini wakati huo pale Nchini Ghana,Taifa ambalo linasifika kwa kuwa na Jeshi Imara Afrika,Mwanamke wa kwanza katika historia ya Ghana,Kamanda Constance Efunu, alikuwa anateuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ghana.

Ajenda ya jinsia kwa sasa ndio ajenda kubwa ya kimaendeleo endelevu duniani bila kuibeba lazima tutaachwa nyuma, lazima Rais Samia Suluhu Hassan, aungwe mkono kwa nguvu zote katika ajenda hii ya kistratejia!

+255746726484
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %