0 0
Read Time:4 Minute, 14 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
Octoba 22,2021.

Kama tunataka kuheshimika kama Taifa”National Reputation” ,lazima heshima yetu ijengwe kuanzia ndani kwenda nje ya mipaka yetu na sio kinyume chake na hiki sio kitu kipya tangia enzi za Mwalimu JK Nyerere ambapo tulianza kujenga heshima yetu ndani ya mipaka yetu na kuanza kutanuka na kuweza kusikilizwa na wengine hasa barani Afrika.

Wakati juzi tu Watanzania tulikuwa tukimuenzi Baba wa Taifa hili, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wakati huo ajenda zake za wazi wazi kuhusu “Pan Africanism” ni kama zimetuponyoka na tumeanza kukumbatia ubeberu kwa nguvu zetu zote!

Kama kuna kitu Serikali ya awamu ya tano ya JPM iliweza kukitumia vizuri na kujijengea umaarufu kwa wapiga kura wa Tanzania na kuweza kuwa na ushawishi mkubwa katika Siasa za Afrika ndani ya miaka yake mitano, basi ilikuwa ni “disconnecting Tanzania from dependency” angalau kwa maneno tu”..Tanzania ni tajiri,tupo kwenye direction nzuri,hakuna wa kutuchezea,tutafanya wenyewe,waje wanalia waje wanachekaa nimesema hapana………….”.

Ni wazi kuwa tusipokuwa makini na ajenda hii,kipimo chetu kwa wapiga kura wetu mwaka 2025 hakitakuwa ni maendeleo gani tumewapa ndani ya miaka minne ya utawala wetu bali swali lao kubwa litakuwa je,yapo wapi mambo tuliyokubaliana kuyasimamia kama Taifa dhidi ya utu na heshima yetu?

Inawezekana hakuna au ni wachache wataokwambia haya Rais wangu na Mama yangu, Samia Suluhu Hassan lakini kwa mapenzi makubwa lazima niyaseme haya kwani mimi ni mmoja ya wanaCCM ambao nimeamua kusimama na wewe mpaka mwaka 2030 utakapokuwa unampa mwanaccm kijiti hiki tena.

AJENDA ZIPI ZA JPM ZINAWEZA KUTUVURUGA?

Msema kweli ni mpenzi wa mungu,maneno yako siku unazindua mpango wa maendeleo wa Taifa kuhusu matumizi ya fedha za IMF na wapi unataka kuzielekeza,Mama yangu ulisema,Nanukuu;

“…JPM alikuwa mtu wa kipekee sana na mpaka sasa viatu vyake ni ngumu kunitosha……”.Nukuu hii inaweza isiwe rasmi sana lakini hayaendi mbali na maneno yako ya dhati kabisa uliyoyasema.

Moja ya ajenda ambayo inaweza ikatubebesha gharama kubwa kuelekea mwaka 2025 ni ajenda ya UVIKO 19 lakini bahati mbaya sana wanaccm hatutaki kuisema kwa kuogopa kupoteza mikate yetu kwako.

Jarida la African Report, huko kwenye mitandao limeendelea kuwavuruga Watanzania na wanaccm bahati mbaya sana hakuna anayejibu hoja hii nzito ambayo sio tu inamaka matope heshima yetu ndani ya bara la Afrika bali pia inaweza kutupoteza uhalali wetu kwa kiasi fulani kwa wapiga kura wetu!

Serikali yoyote makini duniani uendeshwa na “public Opinion” ndio maana wajibu wetu kwako lazima uwe kuweka mezani “public opinions” hizo kwa lengo la kukisaidia Chama na Serikali yetu pendwa ya CCM ya awamu ya sita.

Gharama ya “kudismiss” hofu hii kubwa ni kubwa kuliko gharama ya kukubali hofu hii na kuifanyia kazi haraka kwa maslahi mapana ya Chama changu na Serikali yake kuelekea 2025.

Jarida la African Report la hivi karibuni linasema na nitanukuu kwa kiswahili;

“…Serikali ya Tanzania imemkodisha Waziri Mkuu wa zamani wa Uwingereza Tony Blair katika shughuli maalum mbili;(i)kuwa mshauri wa Rais Samia katika masuala ya uviko 19 na pia (ii) kuwezesha kurudisha sura nzuri ya Tanzania iliyopotea……”.

Kwa mujibu wa ICIJ repoti ya Octoba 3,2021,inamtaja kwa jina Waziri Mkuu Mstaafu,Tony Blair kama miongoni mwa viongozi wastaafu waliojipatia fedha nyingi kwa njia haramu akiwemo pia Uhuru Kinyatta wa Kenya.Taasisi ya kimataifa ya wanahabari za Uchunguzi(ICIJ), imeendelea kusema kuwa,zaidi ya Trilioni mbili za kitanzania, zinamilikiwa na viongozi wa kisiasa wa sasa na wastaafu duniani!Je,uhalali wa ndugu Tony Blair kuipaka mafuta “image” ya Tanzania unatoka wapi?

Taarifa hii ya Tony Blair na Tanzania, kwa kifupi imeleta taharuki kubwa hasa kwa Nchi ambazo zimekuwa zikiiona Nchi ya Tanzania kama kioo cha ukombozi wa bara nzima la kifikra na kifalsafa”Pan -Africanism”.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Mstaafu huyo wa Uingereza,Tony Blair amefanya ziara mbili Nchini, zote zikiwa na dhima ya kusaidia Tanzania kupambana na uviko – 19 kupitia taasisi yake ya Instititute for Global Change.Je,Tony Blair ni mfanyabiashara kwa sasa au anatumika?

Heshima hii tuliyoitengeneza kuanzia Mwalimu Julias Kambarage Nyerere mpaka sasa tikiipoteza gharama yake ni kubwa mno kuibeba!Trust Me!

Taarifa ya TANAFRICA TV ya Jana, moja ya media ya huko Uingereza ambayo imejipambanua kuipigania Serikali ya CCM tangia awamu ya tano na awamu ya sita, imeshutumu wazi wazi kuhusu mpango wetu huo kama kweli hupo!

Ni wazi kuwa “image” ya Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe kama ambavyo Mwalimu Nyerere na JPM walifanya na wakaweza!Kuaminishwa kwamba “image” ya Taifa hili ilipotezwa na JPM ni kujitafutia balaa kubwa kwa Watanzania masikini!

Kama kuna ukweli kuhusu taarifa hii ya THE AFRICA REPORT,basi vyombo husika vinapaswa kuja kuondoa harufu hii mbaya kwani tunaoshinda mitandaoni tunajua “what is going on” na tukikaa kimya ni kuisaliti Serikali yangu ya CCM na kumsaliti Rais wangu!

“..nitasema kweli daima,fitina kwangu ni mwiko…..”.

Mwandishi ni Mwana majumui wa Afrika,kijana wa CCM,makamu Rais wa zamani,Daruso-IJMC,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari -Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani,vyuo vikuu vya Saut-Tabora na Tumaini Iringa na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+225746726484.
+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %