
Kilele cha wiki ya umoja wa Wanawake Tanzania kufanyika IKWIRIRI MKOA WA PWANI ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan. Katika sherehe hizo ataenziwa mwanamke shujaa wa Taifa letu Bi Titi Mohammed, mmoja wa wanaharakati katika mapambano ya kudai uhuru wetu.