Read Time:1 Minute, 0 Second
NUKUU ZA RAIS SAMIA
“Tumekutana hapa kwa madhumuni makuu mawili, moja ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya UWT Kitaifa na jambo la pili ni kumuenzi Hayati Bibi Titi Mohamed na tena aenziwe hapa nyumbani kwake Rufiji”
“Historia ya Bibi Titi Mohamed imeandikwa katika kurasa chache sidhani kama imetosha. Nitoe rai kwa watafiti na waandishi wa masuala ya siasa na jamii wafanye hivyo ili jamii iweze kuujua mchango wa marehemu Bibi Titi Mohamed kwa jamii na Taifa”
“Tumekusanyika hapa si tu kumsifu ili tumsifu, bali tumsifu kwa lengo la kwenda kujipaga kwa matendo yetu yaendane na dhamira ya shujaa wetu huyu Marehemu Bibi Titi” Rais Samia Suluhu Hassan
“Wito wangu kwa wanawake, kuendelea kuwa wamoja na kurekebishana mapungufu tuliyonayo kwa njia ya vikao na njia za kistaarabu,” Rais samia Suluhu Hassan “Biblia imetupa ruhusa wanawake tuseme, lakini kwenye Biblia tuliambiwa tuseme mema, sasa wanawake sisi hatuitumii vyema hiyo fursa, Biblia imetutuma tubebe mema tuyatangaze kwa watu, sisi tunakwenda kutangaziana uovu, kuzushiana majungu na kusambaza umbea,”- Rais Samia “Sasa naomba mjue kwamba hiyo ni dhambi, turudi kwenye maagizo ya Biblia lakini nina hakika dini zote zimetuelekeza hivyo kusema yaliyo mazuri na tusiseme yale ya uongo, majungu, uzushi na kusambaziana yasiyokuwepo,”- Rais Samia
#WikiYaUWT
Happy
0
0 %
Sad
0
0 %
Excited
0
0 %
Sleepy
0
0 %
Angry
0
0 %
Surprise
0
0 %