BILIONI 32.2 KUJENGA NA KUKARABATI SOKO LA KARIAKOO – WAZIRI UMMY
# Ampongeza RC Makalla kwa kusimamia zoezi vema la kuwapanga Wamachinga na Jiji kuwa safi
# Ataja kujengwa Soko dogo kwa ghorofa Sita juu na mbili chini Aidha Asisitiza Kipaumbele kutolewa kwa waliokuwa Wanafanya Biashara hapo kwanza
# Naibu Waziri wa Fedha asema Fedha zipo tayari zitakapohitajika muda wowote zinatoka
#RC Makalla kwa niaba ya RAS akiri kupokea maelekezo ya kuziomba Fedha hizo kwa Katibu Mkuu
# Kiongozi wa Wamachinga DSM Ampongeza RAIS kwa jitihada zote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 32.2 Kujenga na Kukarabati Soko la Kariakoo
Hayo yamesemwa Leo tarehe 6 Novemba 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. UMMY Mwalimu alipotembelea Soko la Kariakoo ili Kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais
Akiwa hapo Mhe. Ummy amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanikisha vema zoezi la kuwapanga Wamachinga na kufanya Mji kuwa safi
Waziri Ummy ameeleza kuwa Kiasi Cha Shilingi Bilioni 26.6 kimetengwa ili Kujenga Soko dogo lenye ghorofa Sita kwenda juu na ghorofa mbili kwenda chini litakalochukua Wafanyabiashara 2200 aidha, kiasi Cha Shilingi Bilioni 6 kimetengwa ili kukarabati Soko lililoungua na kusisitiza kipaumbe kitolewe kwa wale waliokuwa Wanafanya Biashara hapo
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamadi Masauni amesema kuwa Fedha zipo tayari na pindi zitakapohitajika zitapatikana
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kwa niaba ya RAS amekiri kupokea maelekezo ya kuziomba fedha hizo kwa Katibu Mkuu Tamisemi ili kujenga na kukarabati Soko la Kariakoo
Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Ndg. Steven Lusinde amempongeza Rais Samia kwa kuwa Mstari wa mbele kuboresha Mazingira ya Wamachinga na kuahidi kutoa Ushirikiano pindi wanapohitajika
Ikumbukwe kuwa tarehe 10 Julai 2021 Soko la Kariakoo liliungua na Leo hii Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi hicho Cha Fedha ili wafanyabiashara wafanye Biashara katika Mazingira yanayofaa