0 0
Read Time:55 Second

Dodoma.

WU®

WABONGO UGHAIBUNI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kwa kuwa suala la uraia pacha linahitaji mchakato wa kikatiba kwasasa wataanza utaratibu wa utoaji wa hadhi maalumu (special Status) kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni.

Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 20, 2021 wakati akizungumzia mafanikio ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

“Sasa tunaondoka kwenye uraia pacha tunaingia katika hati maalum ambayo tunaona kuwa itatuvusha. Kama unavyojua uraia pacha ni mchakato wa kikatiba,”amesema.

Amesema amesoma na kuelewa utaratibu wa utoaji wa hati maalum unaotumika katika nchi nyingine ikiwemo India ambao ndio njia mbadala ya kuweza kutambua mchango wao na haki ambayo wamekuwa hawapati katoka kipindi hiki.

Aidha, Balozi Mulamula amesema mwaka 1962 mara baada ya uhuru kupatikana walikuwa na balozi mbili tu katika nchi za Uingereza na Umoja wa Mataifa nchini Marekani lakini hadi sasa wanabalozi 44 na balozi ndogo sita.

Amesema hivi karibuni wakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wamefungua Balozi ya Vienna na baadaye watafungua Jakata nchini Indonesia.

Amesema pia mafanikio mengine ni Tanzania kuwa wenyeji wa balozi 62 nchin

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %