0 0
Read Time:5 Minute, 14 Second
Jicho la Uledi

George Michael Uledi
Kyela,Mbeya.
January 17, 2022.

Wakati vikao rasmi vya kuchakata majina ya watia nia ndani ya CCM kwa nafasi ya Uspika vikianza kesho,mwanachama yoyote atakaye teuliwa na Chama kupeperusha bendera ya CCM kuna mambo Lazima yawepo kichwani kwake!

Ni wazi kuwa vikao vya mchujo vya safari hii uenda vikawa vigumu zaidi kwa maana ya kuwa na vigezo ambapo mchakato wa safari hii unaweza kuangalia zaidi vigezo vya kawaida vya jinsia ya mgombea,uzoefu wa mgombea na weledi wa mgombea!

CCM itaangalia mgombea ambaye anaweza “kubalance” kwa viwango vya juu mambo makuu matatu kwa wakati mmoja ambayo ni(i)maslahi mapana ya CCM (ii)maslahi ya Serikali ya CCM pamoja na(iii)maslahi ya Bunge kama chombo cha wananchi wa Tanzania!

Mgombea wetu wa CCM nafasi ya Uspika lazima ajue kucheza na mambo makuu mengine makubwa matatu katika kuliongoza Bunge letu!

Kwa mujibu wa vitabu vya uongozi jeshini,kuna aina tatu za”Leadership Styles” kumuongoza kiongozi katika kufikia maamuzi yoyote yale yawe ya kisiasa,kiuchumi, na hata ya kijamii;

1.Boss type of a leadership!Spika wetu wa CCM lazima ajue kuwa pamoja na kwamba Bunge ni sehemu ya uwakilishi wa wananchi lakini wakati mwingine Bunge linapaswa kusimama na Serikali dhidi ya wananchi katika kusukuma ajenda nzito za maendeleo ya watu wetu mbele!

Sio lazima kila wakati maamuzi ya Serikali yaungwe mkono na wananchi wote kwahiyo lazima Spika wetu ajue kuwa kuna wakati atalazimika kusukuma maamuzi ya Serikali hata kama wananchi hawayataki “as long as” yana maslahi mapana kwa Taifa!

Staili hii ya uongozi hutumika pale ambapo kiongozi unakuwa unajua faida ya maamuzi yako lakini watu wako unaowaongoza wakawa wamekosa taarifa sahihi kuhusu jambo husika!kiongozi lazima ukubali kuwa hawezi ukawafurahisha watu wote kila wakati lakini unapaswa kufanya maamuzi kwa maslahi yao ya mbele na maslahi ya Taifa!

2.Pursueder type of leadership!Ni wazi kuwa tunahitaji aina ya Spika mwenye uwezo wa kushawishi na mjenzi mzuri wa hoja!Ni vizuri Spika wetu ajue kuandaa na kutengeneza mijadala Bungeni ambayo inaweza kutengeneza uhalali wa maamuzi ya Serikali au Bunge kuhusu mambo ya maendeleo!

Spika wa Bunge letu safari hii lazima ajue kushawishi umma na wabunge kwa kutumia hoja nzito na halali kuhusu maamuzi ya Serikali!kuna wakati mipango mingi ya Serikali inapigiwa kelele sababu ya wananchi kukosa taarifa sahihi tu kwahiyo tunahitaji Spika mwenye ushawishi wa hali ya juu!Samweli Sitta alikuwa na sifa hiyo!

Ni vizuri wakati mwingine Bunge litumike kama sehemu ya ushawishi kwa watu kwa hoja nzito bila kutumia nguvu!Heshima ya Bunge wakati mwingine inatokana na uwezo wake wa kushawishi watu wakubaliane na maamuzi ya Serikali Yao lakini wajibu huo lazima uendane na kuikosoa,kumshauri na kuisimamia Serikali vizuri zaidi!

3. Educator type of leadership!Spika wa Bunge lijalo lazima awe “Mwalimu” wa mambo makuu mawili(I)Parliamentary culture of Commonwealth kwa wabunge wake na (ii) awe ni Spika anayejua “issues” za msingi zinazotawala nyanja za maendeleo,siasa,
uchumi duniani na kuweza kuwapa darasa wabunge na jamii ya kitanzania kwa ujumla!

Mh.Spika mwenye uelewa wa viwango vya juu kuhusu dunia anaweza kuaminika zaidi na watanzania”think globally act locally & vice versa”!Kwa ufupi lazima tuwe na Spika Mwalimu wa kila kitu kinacholetwa mezani kwake kwa ajili ya mijadala!

Spika “fame on issues” unatupa uhalali zaidi ya kuliongoza Bunge na kuweza kuaminika zaidi kwa watanzania!Je,tunakosaje mtu sahihi miongoni mwa watu 70?

SPIKA WETU WA CCM NA THE MUST KNOW!

1.Spika wetu lazima ajue kuwa pamoja na kwamba Bunge ni mhimili “independent” lakini haupo sawa na mhimili mwingine hasa mhimili wa Dola na hasa unapokuwa ni Spika unayetokana na CCM!Ni makosa makubwa Spika kujilinganisha na mhimili wa Dola ambayo inabeba zaidi ya majukumu matatu kwa pamoja yaani (I)Ukuu wa Nchi(ii)Ukuu wa Serikali na (iii) Uamiri jeshi Mkuu!

Kwa namna yoyote ile Spika wetu wa CCM lazima ajue kuwa kuna mhimili mpana zaidi yake pamoja na ukweli kuwa mhimili yote mitatu IPO huru!

Suala la kujua mipaka yako dhidi ya mihimili mingine ni suala la msingi zaidi kwa Spika ajaye!Hatutaki kurudia makosa ya nyuma tena!

2.Spika wetu wa CCM lazima ajue kuwa yeye Kwa utaratibu anatokana na CCM na nafasi yake ya Uspika imepatikana kwa sababu ya CCM kwahiyo suala la “kubalance” maslahi mezani kwake haliepukiki!Maslahi ya CCM,maslahi ya Bunge na maslahi ya Serikali lazima yaende pamoja bila kugongana!Failure to do so itakuwa tatizo kubwa kwake!

3.Spika wetu lazima ajue kuwa Bunge la CCM lenye wabunge zaidi ya 95+ wa CCM ni lazima liwe “mbwa anayeng’ata na sio mbwa anayebweka”!Spika wetu lazima ajue kuwa kwa mazingira tuliyonayo ya kuwa na karibia asilimia 95+ ya Wabunge wa CCM lazima tuwe na kitu kinaitwa”self regulatory system”.

Bunge letu la sasa halipaswi kwenda kuisifia Serikali yetu kila wakati kwani kufanya hivyo ni kuibomoa Serikali ya awamu ya SITA kuelekea 2025!Uwingi wetu huu lazima umfanye Spika kujua kucheza na dhana ya “parliamentary self regulation” kwa lengo kuisaidia Serikali kwa kufanya Ile “watch dog roles”!Kuepuka gharama za kutokuwa na upinzani Bungeni tusione kama fursa nzuri kisiasa bali tuone ni hasara katika siasa za kisasa”contemporary politics”.

Afya ya mijadala Bungeni lazima irudi sasa kwa maslahi mapana ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025!Serikali ya CCM ikikosolewa na wabunge wa CCM ndani ya Bunge ni afya zaidi kuliko Serikali ya CCM kukosolewa na watu nje ya Bunge!

Ni wazi kuwa vyama vya upinzani kwa sasa vipo katika “agenda stocking” kuelekea Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,ni wazi kuwa kutoruhusu mijadala Bungeni ni kuendelea kuwapa nafasi wapinzani ya kufanya “agenda stocking” kuelekea 2025 na njia pekee ya kuwabana ni kwa CCM yenyewe kupitia Bunge letu kuanza kuhoji hoja hizo!Spika wetu wa CCM anapaswa kuzingatia hapa ni “kiasi” na levels za mijadala ndani ya Bunge lake!

NATARAJIA vikao vya ndani ya chama vitakuja na mtu anaweza kubeba mabegani maslahi yote matatu kwa maana ya maslahi ya CCM,maslahi ya Serikali na maslahi ya Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa Habari wa zamani,Idara ya Habari -Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo Cha Maofisa wa jeshi Monduli Arusha,Mhadhiri Msaidizi wa zamani, vyuo vikuu vya Saut & Chuo Kikuu Iringa na mtia nia ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255784159968.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %