0 0
Read Time:1 Minute, 40 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AKUTANA NA MSHINDI WA TUZO YA NOBEL YA FASIHI 2021

Ushiriki wa Wazanzibari katika Tuzo tofauti Duniani kutasaidia kuitangaza Zanzibar kwa mataifa mbali mbali pamoja na kukuza Uchumi wake.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alipokutana na Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi 2021 Profesa Abdulrazak Gurnah alipofika katika Ofisi yake iliyopo Baraza la Wawakiishi Chukwani Jijini Zanzibar.
 
Amesema Tuzo aloipata Profesa Gurnah ni faraja na furaha kwake pamoja na Taifa kwa ujumla ambapo inadhihirisha uwezo na ujuzi walionao Wazanzibari.
Amesema Tuzo hiyo pia ni fursa ya kuitangaza Zanzibar ambapo wageni mbali mbali wataweza kufika Zanzibar kufanya shughuli za kitalii na kupelekea kukuza Uchumi wa Nchi.
 
Mhe. Hemed ameeleza kuwa kukabidhiwa Tuzo hiyo kwa Profesa Gurnah iliamsha hisia ya wazanzibari wengi kufurahia jambo hilo hasa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuthamini Tuzo hiyo na kumpongeza kwa niaba ya wazanzibari.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa tukio hilo litasaidia kuwapa ari hasa Vijana kujituma katika nyanja tofauti ili kupata Tuzo mbali mbali za ndani na nje ya nchi.
 
Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali itatoa mashirikiano ya kila aina kwa wazanzibari watakaoshiriki katika mashindano ya Tuzo mbali mbali ili kusaidia utayari wa Wananchi wake kwa lengo la kuweza kuitangaza Zanzibar na kuiheshimisha kwa mataifa mengine.
 
Nae Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasini 2021 Profesa Abdulrazak Gurnah amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa amefarijika kuona wazanzibari, Waafrika na Dunia kwa ujumla wanafurahia Tuzo hiyo na kueleza kuwa Tuzo hiyo ni ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.
 
Aidha Profesa Gurnah ametoa wito kwa Wazanzibari hasa Vijana kuchangamkia Fursa mbali mbali za masomo zinazotolewa na Nchi jirani na Dunia kwa ujumla ili kuweza kufahamu mengi na kufanikiwa kupata Tuzo mbali mbali.
 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (AMPR)
Mei 27,2022

Imetolewa na Kitengo cha Habari (AMPR)
Mei 27,2022

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %