0 0
Read Time:53 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh.Mahmoud Thabit Kombo leo amekutana na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania Dr. Makakala kuzungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu Watanzania wanaoishi nchini Italia na Ugiriki, “Greece ni moja ya nchi ambazo zinawakilishwa kutoka Italia”

katika mazungumzo hayo Mh Balozi alimfahamisha kamishna mkuu changamoto mbali mbali za Wana Diaspora wanazozikabilina nazo nchini Italia na Ugiriki hasa masuala ya Uhamiaji.

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania, Dr. Anna Makakala alimpokea Balozi Mahamoud Thabit Kombo katika ofisi zake za Makao Makuu ya Uhamiaji Tanzania na kuahidi kufanikisha utatuzi wa changamoto zote hizo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Rome, nchini Italia.

Mh Balozi Mahamoud Thabit Kombo amekuwa akizishughulikia changamoto za Diaspora wake kwa karibu Sana tangu apate uteuzi takriban miezi Saba sasa. Moja ya ahadi zake kwa Diaspora alipokutana nao mara ya mwisho mwezi machi mwaka huu ni kumaliza changamoto zao zinazohusu masuala ya passport hivyo mkutano wake na kamishna mkuu wa uhamiaji unaenda kuondoa tatizo Hilo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
100 %