0 0
Read Time:1 Minute, 2 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameipongeza timu Yanga kwa kutwaa ubingwa wa soka wa Tanzania msimu huu.

Ameyasema hayo leo usiku katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar Es Saalam mara baada ya mchezo ligi Kuu (NBC) ambapo ameyataja mafanikio hayo kuwa ni matunda ya udhamini mkubwa wa kampuni ya GSM, uongozi imara, benchi na wachezaji bora wa Yanga pamoja na mashabiki kwa mshikamano.

”Ilani ya uchaguzi ya CCM ni tuliahidi kuimarisha michezo, soka ikiwa ni sehemu ya michezo hiyo. Serikali ya CCM Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kuboresha viwanja vitano kwa mwaka 2022-2023 kwa mikoa ya Mwanza, Arusha, Tanga, Mbeya na Dodoma kuwa vya kisasa ikiwa ni utekelezaji wa ilani. Mafanikio ya Yanga yawe chachu kwa timu nyingine kufanya vizuri zaidi. Rai yetu kama chama ni kwa makampuni ya kibiashara kujitokeza kwa wingi kudhamini ligi yetu pamoja timu mbalimbali ili kuongeza ushindani zaidi wa ligi yetu” amesema Shaka

Hata hivyo ametoa wito kwa Uongozi wa Yanga kujipanga zaidi ili kuleta mafanikio katika michuano ya kimataifa na hivyo kuzidi kulipa heshima taifa letu kama walivyofanya wenzao wa Simba.

Katika mchezo huo timu Yanga imefanikiwa kuifunga Costal Union 3-0.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %