WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa mashariki, Balozi Liberata Mulamula kabla ya kuondoka nchini Finland ameweza kuongea mengi na Diaspora maarufu Ndugu Edwin Ndaki. Akizungumza na Wabongo ughaibuni Media, Ndugu Ndaki amesema mazungumzo yake na Mh Waziri yamekwenda vizuri Sana maana alipata wasaa wa kumueleza mengi yanayohusu Diaspora Pamoja na ushiriki wao katika Maendeleo ya nchi , kiuchumi na kijamii.