0 0
Read Time:3 Minute, 25 Second
Jicho la Uledi

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

REPOTI ZA MAKUSANYO YA HALMASHAURI ZA INNO KWA MWAKA WA FEDHA 2021-2022 BADO ZINANIFIKILISHA SANA!

George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya.
August 5,2022.

Katika eneo ambalo Mh.Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Mama Samia Suluhu Hassan, anapaswa kutulia ni eneo la uteuzi wa nafasi za Maded,Madas na Madc ambao kweli wanapaswa kuwa na sifa za ziada,uwezo wa ziada na uzalendo wa ziada kwa Taifa na kwa Serikali hii ya awamu ya sita!

Moja ya eneo ambalo nadhani tunapaswa kuchagua watu sahihi kwa maana ya vijana wenye kwanza maono makubwa,ubunifu,uthubutu na njaa ya kutaka kulipeleka Taifa mbele na kwa spidi kubwa, basi ni katika teuzi hizi za maeneo hayo matatu!

Kuna sababu kuu mbili au tatu ambazo zinanifanya nitake kumsihi na kumshauri Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Mama Samia Suluhu Hassan, kabla hajaamua kuachia mkeka wake hivi karibuni!

Moja ni (i)kwamba Serikali yake imekuwa ikipeleka fedha nyingi katika Halmashauri kwa ajili ya kusukuma miradi ya wananchi ya maendeleo ya lakini inaonekana kana kwamba baadhi ya wateule wake hawa Madc,Maded na Madas ni kama vile wameamua kurelux kwa kuona kwamba, fedha inayotoka Serikali kuu inawatosha kusukuma vipaumbele vya maeneo yao!

(ii)Kumekuwepo na ubunifu mdogo katika kutengeneza vyanzo vipya vya mapato kwa wateule hawa wa Rais hivyo mzigo mkubwa kubebwa na Serikali kuu!Wateule hawa wa Mh.Rais, wangeweza kabisa kuisaidia Serikali kuu moja, katika kutengeneza ajira ndogo ndogo kwa vijana kupitia uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kilimo,viwanda na hata maduka katika maeneo yao ya utawala!Kaka yangu Mh.Antony Mtaka alishafanya haya Simiyu,rejea kiwanda cha kuzalisha chaki!

Kama Afande wangu, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Mara ,Meja Generali Selemani Mzee aliweza kuifanya Magereza kuacha utegemezi wa fedha kutoka Serikali kuu,inakuwaje kijana mdogo wa umri wangu ushindwe kubuni vyanzo vipya vya mapato?Shule zetu zinaisaidiaje Serikali yetu ya CCM?

(iii)Inakuwaje kwa Halmashauri mpya ya wilaya ya Mlele leo iweze kukusanya zaidi ya 185% kuliko Mbeya DC?,kuliko hata Ndugu zangu wa Momba,kuliko kwa kaka yangu Mwakiposa kule Mufundi na hata kuliko Halmashauri ya Mbalali?

(IV)Inawezekanaje pale nyumbani kwetu Halmashauri za wilaya za Korogwe leo, ikakusanye 67% ya makisio yake ya Mwaka,same same Tanga, Bumbuli kwa Kaka yangu Makamba pia ikakusanye 58% ya makisio ya makusanyo ya ndani ya mwaka?Wasambaa nani katuroga?

Inakuwaje Halmashauri mbili katika mkoa mmoja”Tanga” ndio zifunge mkia kwa kutofikia makusanyo wakati huo huo Halmashauri mbili yaani Mbulu na Simanjiro katika Mkoa mmoja wa Manyara ndio ziongoze kwa kukusanya mapato kwa ufanisi?Hawa Manyara ni jirani zetu kabisaaa,tumeshindwa hata kuwacopy?

Yaani Mkoa wangu wa Tanga, leo hii eti ndio Halmashauri zake mbili zinafunga mkia kwa kuleta makusanyo ya chini kabisa kabisa kati ya Halmashauri zote Nchini!Hapa ndio anatoka KM wa Tamisemi Prof.Riziki Shemdoe,hapa ndio anatoka Kaka January Makamba,hapa ndio anatoka Oddo Ummy Mwalimu,haiwezekani!
Hivi kweli mpaka leo Ded wangu wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe, ameshindwa kuutafsiri uchumi wa wilaya kama Korogwe kuwa utajiri au kuwa fedha?,yaani wilaya kama Korogwe eti leo inazidiwa makusanyo na Halmashauri ya Mlele?Hapana!

Mimi nadhani kama sisi vijana wa CCM hatuwezi kuifanya hii kazi vizuri ya Udc,uded na udas basi tutafute vijana wenye njaa,maono na uwezo wa kuifanya hii kazi!Sio lazima sana hizi nafasi zije kwetu tu, basi kama vipi tutafute watanzania wengine vijana ambao wamejaa kwenye taasisi za kiraia waweze kutusaidia!alMama Samia alishawahi kusema tunajenga nyumba moja,Tanzania!

Tungekuwa angalau na vijana 60% kwenye local government ambao ni aggressive, leo hii Mama yangu Samia na CCM yetu ingekuwa haina pressure ya mwaka 2025! Personally nakushauri Mama yangu tulia, tumia vyombo vyako vya siri wakutafutie watu sahihi na hii tabia ya kukuchomekea nadhani waache maana kila mkeka unapoletewa lazima ule kichwa kabla ya uapisho!🤣🤣.Hawajifunzi tu!

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kazi Iendeleee!

Mwandishi ni kijana wa CCM,Ofisa wa zamani,Idara ya Habari-Maelezo,Ofisa Mwanafunzi wa zamani,Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli Arusha, Mhadhiri Msaidizi wa zamani,Saut & Tumaini na Mtia nia Ubunge Jimbo la Kyela 2020.

+255746726484.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %