0 0
Read Time:1 Minute, 14 Second

WUยฎ MediaPRODUCTION LIMITED

“MABILIONI YA RAIS SAMIA YAMPA IMANI SHAKA KUWAKOMBOA VIJANA NA WANAWAKE KATIKA KILIMO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema dhamira ya dhati ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuitazama kwa karibu sekta ya kilimo, ikiwemo kuongeza bajeti ya Wizara Kilimo, kutoka sh. Bilioni 254 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sh bilioni 954 sawa na asilimia 224 kwa 2022/2023, italeta mabadiliko makubwa katika uchumi.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kutengeneza fursa nyingi za ajira ambapo kufikia 2025 vijana na wanawake zaidi ya milioni 3 watanufaika na ajira hizo, hatua ambayo imemfanya Shaka atoe muelekeo wa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hususan wasomi wa vyuo vikuu ambao ametaka watambuliwe na kuwezeshwa kupitia kilimo.

Shaka amesema hayo leo Agosti 7, 2022 alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro ambapo amesema kupitia maonesho hayo lipo jambo la faraja ambalo ameliona.

โ€œkuonesha mkazo zaidi katika Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza nguvu kwenye sekta ya Kilimo na dhamira kubwa ikiwa kuwakomboa vijana pamoja na wanawakeโ€.

Aidha amesema kuwa maelekezo ya Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020 – 2025 katika Ibara ya 8 kifungu f imeahidi katika kipindi cha miaka mitano kutazalishwa ajira milioni nane kwa Watanzania, sasa kwenye kutafsiri maelekezo ya Ilani Serikali ya Rais Samia imeshajiwekea mwelekeo ama imeshajiwekea matatarajio yake katika ajira hizo kupitia sekta ya kilimo.

WATCH HERE

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %