
WU® MediaPRODUCTION LIMITED
Mfanyabiashara Mtanzania mwenye kampuni ya ujenzi, anaeishi mjini Genova Italy amefunga ndoa na mwenzi wake siku ya Alhamisi tarehe 1/09/2022.

Ricky Johnson George Bondo ambae pia ni Makamu mwenyekiti wa kamati ya Diaspora nchini Italy, amefunga ndoa mjini Napoli ambako ndiko ukweni kwake. Pamoja na Diaspora kuhudhuria sherehe hizo pia alikuwepo mlezi wa Diaspora ambae ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy , Mh Mahamoud Thabit Kombo ambae aliongozana na mkewe.
Sherehe za harusi zilianzia kanisani ambako walifunga ndoa na Baadae ziliendelea katika kumbi za Villa Vittoria. Mapema baada ya chakula Cha mchana Kabla ya kuondoka na kuendelea na majukumu yake, Mh Balozi aliombwa kutoa neno kama mlezi kwa niaba ya family ya Bondo na baba Mzazi wa bi harusi Anna D’Alessio aliongea kwa niaba ya family yake. Baada ya hapo sherehe ziliendelea mpaka takriban saa nne ya usiku.










