0 0
Read Time:1 Minute, 32 Second

WU® MediaPRODUCTION LIMITED

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehitimisha Tamasha la Siku ya Kizimkazi akiagiza tamasha hilo kufanyika kwa mzunguko sehemu mbalimbali za wilaya ya Kusini ili kuwapa fursa Zaidi wakazi wengi wa Zanzibar kushiriki na kujifunza masuala kadha wa kadha kupitia michezo na maonesho ya huduma na shughuli mbalimbali za taasisi na bianafusi yanayo oneshwa kama sehemu ya tamasha la siku ya kizimkazi.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo September 3, 2022 akiwa Kizimkazi wilaya ya Kusini Visiwani Zanzibar wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa Zanzibar waliofurika katika viwanja vya Kizimkazi, kushiriki kilele cha tamasha la siku ya kizimkazi.

Rais Samia amesema, tamasha hilo lililodumu kwa muda wa siku saba kuanzia Augost 29 hadi September 3, 2022, kwa sasa limekua na Sura ya Kiwilaya na kuagiza waandaaji wa kuhakikisha linafanyika sehemu mbalimbali za wilaya ya kusini ili kuwapa nafasi wasioweza kufika Kizimkazi kunufaika na tamasha hilo katika maeneo yao.

“Faraja yangu leo ni kuona kuwa tamasha hili sasa limekuwa na sura ya Wilaya, jina linabaki kuwa lilelile Kizimkazi lakini ukweli ni kuwa hili kwa sasa ni tamasha la wilaya au mkoa mzima wa Kusini” alisema Rais Samia.

Akielezea historia na dhamira ya kuanzishwa kwa tamasha hilo Rais Samia amesema kuwa nia ilikuwa ni kuwaleta Pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Kizimkazi na maeneo ya Jirani, na watanzania kwa ujumla.

Aidha lengo la pili lilikuwa ni kulinda, kudumisha na kuzilisisha mira, tamaduni na desturi za wakazi wa Mkoa wa Kusini kwa kizazi cha leo na kijacho, huku lengo la tatu likiwa ni kuhamasisha shughuli za maendeleo, kwa njia mbalimbali ikiwemo kutangaza fursa za kiuchumi, zilizopo ndani ya wilaya na mkoa wa Kusini.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ni miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania walioshiriki katika sherehe za kilele cha siku hiyo.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %