
WU® MEDIA
Na Dr Yahya Msangi
SHAMBA LA KOROSHO JIMBO LA KERALA INDIA: KOROSHO TAMU LAKINIII…..!
Jimboni Kerala kuna shamba la kampuni ya Kasaragond Cashew Plantation. Ndilo lilikuwa shamba kubwa la korosho nchini India miaka île ya 1940s – 1970s. Lilianzishwa na bepari McKenzie enzi ya ukoloni wa Waingereza.
Kwa miaka kadhaa lilikuwa likinyunyiza sumu (mnaita viatilifu aka pembejeo) aina ya organophosphate. Siku si nyingi wakulima kule Mtwara walidai simu hii aina ya Sulfur iliingizwa ikiwa tayari ime expire. Wizara ikadai itamshughulikia muingizaji.
Ukweli ni kwamba hâta Ukiwa fresh matokeo ndiyo haya unayoona kwenye picha hizi. Kuanzia 2003 -2007 nilikuwa Mratibu WA mradi ukiitwa GLOBAL PESTICIDES PROJECT uliofadhiliwa na SIDA (Sweden). Nikizunguka dunia nzima kufundisha madhara ya sum za Kilimo kwa afya ya binadamu na mazingira. Pia nikikagua utekelezaji wa mkataba wa ILO number 170 wa mwaka 1990 (ILO CONVENTION ON CHEMICAL SAFETY IN WORPLACES). Nikifundisha Afrika, Ulaya, Asia, America kusini.
Safari moja nikafika Kerala India. Nikakutana na hili shamba la korosho. Kwa miaka mingi wakinyunyuza sumu kwa kutumia helikopta kutokana na ukubwa wa shamba. Helikopta ikimwaga sumu mpaka mashuleni, majumbani, visima vya maji, mtoni, n.k. Dhumumi kunywa kudhibiti gonjwa la ukungu kwenye mikorosho. Sawa na Mtwara tofauti ni kuwa Mtwara hawatumii helikopta bali mabomba (knapsack) ya kubeba mgongoni. Mara nyingi yanavuja mgongoni mwa mbebaji analowana chapachapa.
Mara nyingi wanaonyunyiza hawana kivazi cha Kinga au wanakula au kuvuta huku wananyunyiza. Mara nyingine wanachanganya sulfur kwa viganja. Mbaya zaidi wanatumia makopo yaliyohifadhi sulfur kwa kuhifadhi maji, maziwa, unga au nafaka.
Utasikia wizara na wanaharakati wakidai “Mwaka huu tutapeleka sulfur ya kutosha Mtwara kabla ya msimu kuanza”! Au “Serikali ipeleka haraka sulfur kuepuka hasara kwa wakulima”! Kamwe hutasikia “serikali itatoa haraka elimu kwa wakulima kuhusu madhara ya sulfur”! Masikini wakulima! Wanashukuru kwa kuletewa sulfur ya kutosha! Wangelijua madhara yake huenda wangeandamana kudai vifaa ya Kinga, elimu, matibabu, n.k.
Namsikilizaga Zitto “akitetea” wakulima wa korosho kwamba wapelekewe sulfur haraka ! Najua dhahiri hajui chochote kuhusu ukali (toxicity) ya sulfur! Angedai kwanza elimu au sumu mmbadala. Zipo! Sio salama lakini ni afadhali ukilinganisha na sulfur.

Huyu Binti mrembo utadhani ameota titi. La hasha! Ni uvimbe wa kansa ya titi. Breast cancer. Kaipata utotoni. Hawa watoto waliosimama ukutani hawana akili hâta chembe. Ni makolo ya kihindi! Hawaelewi chochote darasani. 1+1 ni ngapiii? Yanajibu chochote. Miaaa, selasiniii! Walimu wamefundisha wee, tuisheni weee lakini waaapi. Ukilituma dukani ulikiandikie karatasi. Bila hivyo utashangaa karudi kuuliza “mama ulinituma ninunue nini vileee”! Hâta mara 5. Litaenda litarudi kuuliza.

Hawa Wenye ulemavu waliupata tumboni kwa mama Zao. Organophosphate inaweza kuingilia ukuaji wa mtoto tumboni mwa mama. Ina SIFA 2 kipare zinaitwa “endocrine disruption” na “cholinesterase inhibition”. Endocrine ni tezi inayosimamia ukuaji “growth & development” mtoto Akiwa tumboni kwa mama. Cholinesterase ni “enzyme” ambayo inasimamia mawasiliano baina ya mama na kichanga tumboni. Inachofanya sulfur au organophosphate yôyote ni kuingilia mawasiliano hayo. Mfano inageuza meseji ya “ota vidole vitano Kila mkono” n’a kuifanya matoto aisome hivi “ota vidole viwili kila mkono”. Mwili wa kichanga utadaka hii meseji feki. Atazaliwa mlemavu kadri ujumbe ulivyochezewa.
Nilibahatika kuwatembelea hawa watoto. Wengine tuliwasaidia. Kama huyu WA mguu tuligharamia operesheni ya kukata huo wa kulia na kumpa mguu bandia. Hii ilimwezesha kutembea kwenda shule.

Ushauri: wizara isijikite tu kupeleka sumu kwa wakulima. Ujikite Pia kutoa elimu na vazi la kinga kwa wakulima na walaji.
Onyo: unapobugia korosho au ulaka ukumbuke ilinyunyiziwa Sulfur. Watu wanaweza kudhurika shule ikagoma wakakimbilia umachinga. Saa ingine sio Kosa lao. Wamebugia Sulfur! Najua Ntwara korosho ni viagra! Shauri yenu!
“Makofi tafadhali kwa mlamba asali aka TICHA.“








