0 0
Read Time:3 Minute, 20 Second

Maonesho yalianza 11-12-12-13 March, 2023

Fermo, Marche IT.

Tan Warriors Wasaini mikataba yenye fursa kubwa kwa Vijana wa TANZANIA

TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY KUWA KITUO KIKUBWA CHA MICHEZO AFRIKA YA MASHARIKI

Tarehe 11-12-13 March 2023 Tanzania ilishiriki maonesho ya kimataifa ya biashara yaliyofanyika mji wa FERMO mkoani MARCHE nchini Italy. Katika maonesho hayo makubwa ushiriki wa Tanzania ukiongozwa na kuratibiwa vyema na Ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Katika maonesho hayo ya kibiashara ambapo mwaka huu ilichaguliwa Tanzania kushiriki kama Nchi ya Afrika.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Ascoli dada Anna Minja akishiriki kwenye Banda la TANZANIA kutoa maelezo mbalimbali ya bidhaa za Tanzania.Diaspora wameweza kutoa mchango Mkubwa hasa kwenye Mawasiliano ya lugha. Vile Mkurugenzi wa Trinity Southern Sahara alishiriki pia kuitangaza Tanzania Kupitia mavazi ya asili ya kabila lake la Mmasai na ilikuwa kivutio kikubwa na hamasa kwa Waitaliani kutamani kutembelea TANZANIA.
Mkurugenzi Mainga Ole Kalaita akitoa zawadi kwa Wataliani katika kutangaza nchi yetu kupitia sanaa na utamaduni wa Tanzania.

Pamoja na bidhaa mbalimbali za Tanzania kuoneshwa na kutangazwa katika maonesho hayo, pia Tanzania ilipewa nafasi ya kuonyesha mapishi ya chakula katika maonesho na pia kuweza kuandaa CHAKULA Rasmi Cha jioni ambapo walihudhuria viongozi mbalimbali akiwemo Mstahiki Meya wa FERMO akiambatana na viongozi na wananchi walioalikwa.

Katika HAFLA hiyo ya chakula Cha jioni Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo alipata nafasi ya kuongea na wageni waalikwa, Mh Balozi alitoa shukran kwa Tanzania kupata nafasi hiyo adhimu kushiriki katika maonesho na kuitangaza Tanzania kibiashara, uwekezaji,Mila na utamaduni. Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umeleta matokeo chanya kwani Mh Balozi alialikwa na kutembelea Chuo Kikuu Cha CAMERINO.

Mh Balozi Pichani akiwa na mkewe
Picha ya Pamoja Mh Balozi na Ujumbe wake wakiwa na mkuu wa Chuo

Chuoni hapo alipokelewa na mkuu wa Chuo hicho Balozi Mahamoud Thabit Kombo akiwa kaongozana na Mkewe Pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Diaspora nchini Italy Ndugu Kagutta Maulidi, Dada Eva Nangela ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania mji wa Genova Italy ambae pia ni Mratibu (coodinator) wa Tan Warrious Sports Academy, pia alikuwepo mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Napoli Ndugu Salim Awadh, baada ya mazungumzo mafupi mkuu wa Chuo na Mh Balozi walifanya ziara ya kutembelea majengo na vitengo mbalimbali vya Chuo hicho chenye historia kubwa tangu kianzishwe mwaka 1336.

Kwa umuhimu wa pekee katika ziara hiyo hapo chuoni Mh Balozi aliongozana na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Trinity Southern Sahara na Tan Warrious Sports Academy Ndugu Mainga Ole Kalaita aliye ambatana na Mkurugenzi wa ufundi wa Sports Academy hiyo Ndugu Suleiman Khalid Sharrif. Mapema siku hiyo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisaini mikataba miwili mikubwa, mmoja ulikuwa ni wa ujenzi wa miundombinu ya Sports Academy ambayo itakuwa ya viwango vya kimataifa, pia Tan Warrious ilisaini mkataba na Chuo hicho kikuu Cha CAMERINO kushirikiana katika kutoa fursa za vijana wenye vipaji kushiriki katika mafunzo na elimu ya juu. TAN WARRIORS SPORTS ACADEMY ipo mjini MOROGORO inategemewa kuwa kituo kikubwa Africa ya mashariki kitakachokuza vipaji na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya michezo Tanzania.

Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Trinity Southern Sahara Mh. Mainga Ole Kalaita akisaini moja ya makubaliano
Balozi wa Tanzania nchini Italy Mh Mahamoud Thabit Kombo akushuhudia utiaji Saini kati ya Tan Warrious Sports Academy na wadau nchini Italy Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa Tan Warrious Sports Academy ndugu Mainga Ole Kalaita, Mkurugenzi wa Ufundi Suleiman Khalid Sharrif na Mratibu (Coodinator) wa Tan Warrious Sports Academy Madam Eva Nangela.

Mh Balozi Mahamoud Thabit Kombo akiongozana na Diaspora Pamoja na Mkurugenzi wa Trinity Southern Sahara Ndugu Mainga Ole Kalaita walitembelea kiwanda kikubwa cha kuchakata Tumbaku na uzalishaji wa Sigara.

Mkurugenzi Ole Kalaita akisalimiana na wenyeji kiwandani hapo
Mh balozi akipokelewa kiwandani
Mh Balozi akipatiwa maelezo na historia fupi ya kiwanda hicho chenye takriban miaka mia tatu
Kabla ya kuagana na uongozi wa kiwanda Cha Tumbaku , Mh Balozi na Ujumbe wake wakipata kahawa, pembeni ni Mama Balozi
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
100 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %