
BOXING THE ROAD TO PARIS FRANCE
Na Mwandishi wetu
GFAMILY KAGUTTA

Bondia wa Tanzania Yusufu Luccasi Changarawe usiku huu ameing’arisha Tanzania baada ya kushinda pambano la kutafuta kufuzu kushiriki kwenye mashindanoi ya Olympic nchini Paris yatakayofanyika mwaka huu 2024.
Changarawe ambae anapigana Light Heavy Kilo 80, ameshinda kwa knock out raundi ya kwanza katika ya kwanza na ushee kwa kumpelekea ngumi nzito bondia wa Venezuela.
Bondia wa Venezuela aliingia kwa kishindo na kujaribu kumchanganya Yusufu Changarawe ambae alionyesha utulivu wa hali juu kudhihirisha uzoefu na mbinu alizonazo za mchezo wa ngumi.
“Bondia wa Venezuela Pereira ni mzuri sana na ilikuwa vigumu kumsoma maana sikuwahi kumuona hata kwenye mitandao” ..alisema Yusufu Wakati akiongea na Wabongo Ughaibuni Media.
Yusuf Changarawe anaingia tena ulingoni tarehe 8/03/2024 kupambana na bondia wa Norway
Bondia wa Tanzania ameongozana na mwalimu Coach Mohamed Abubakari Mohamed na Makamu wa Rais wa kamati ya Olympic Tanzania Mh. Henry Benny Tandau

