0 0
Read Time:1 Minute, 40 Second

Busto Arsizio VA Italy

Na Nsangu Kagutta

Bondia wa Taifa ambae yupo katika kugombea nafasi ya kushiriki katika michezo ya Olympic mwaka huu itakayofanyika kuanzia mwezi wa saba Paris Ufaransa, Yusufu Luccasi Changalawe leo tarehe 8/03/2024 anapanda ulingoni kupambana na bondia Gedminas Mindaugas kutoka Norway

Katika picha ya pamoja Makamu wa Rais wa kamati ya olympic MH. Henry Benny Tandau akiwa na Bondia wa Taifa Yusufu Changalawe na Coach Mohamed Abubakari Mohamed walipokutana na Wabongo ughaibuni Media kabla ya pambano la kwanza dhidi ya Bondia wa Venezuela

Yusufu Changalawe anaingia ulingoni baada ya kumtwanga kwa knockout bondia Pereira Diego kutoka Venezuela siku ya tarehe 4/03/2024 katika viwanja vya Busto Arsizio nchini Italy.

Nae Bondia wa Norway anaingia uliongoni baada ya kushinda kwa point dhidi ya bondia wa Argentina siku hiyo hiyo ya tarehe 4/03/2024.

Akiongea na Wabongo Ughaibuni Media baada ya kumtwanga Diego wa Venezuela, Bondia wa Taifa Yusufu Changalawe alisema hana wasiwasi na mnorway kwa sababu alimuona wakati akipigana hivyo alisisitiza watanzania kuendelea kumuombea. Nae Mwalimu alieambatana na Yusufu Changalawe, Coach Mohamed Abubakari Mohamed alisema amemuandaa vyema bondia wake hivyo hana shaka kabisa nae aliwataka na kuwaomba watanzania kumuombea bondia wa taifa ili aweze kuiwakilisha vyema nchi yake. Katika msafara huo unaongozwa na Makamu wa Rais wa Kamati y a Olympic MH. Henry Benny Tandau nae aliongea machache kuhusu changamoto za michezo kwa ujumla na ushiriki wa Tanzania katika michezo ya kimataifa hasa Olympic, alisema bado inahitajika ushirikiano zaidi na taasisi zote za michezo Tanzania ili kuongeza ufanisi na kupata nafasi zaidi kwa wachezaji kuwakilisha Taifa. Makamu wa rais wa kamati ya Olympic Tanzania alisema anaridhishwa sana na hali ya bondia wa taifa na ana uhakika anaweza kushinda kuelekea Paris France mwaka huu.

Mh Tandau amewashukuru sana Wabongo Ughaibuni Media kuungana nao , kuwatia moyo na kuwapa taarifa Watanzania kuhusu tukio zima la mashindano hayo yanaitwa ROAD TO PARIS, Wabongo ughaibuni Medi ndio media pekee ya kitanzania iliyokuwepo kwenye tukio.

Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleepy
Sleepy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %