
Balozi wa Tanzania The Hague ashiriki kutangaza utamaduni wa Mtanzania kwenye mavazi

Sherehe za Embassy Festival zinazofanyika kila mwaka nchini Netherland zinashirikisha balozi za nchi mbalimbali duniani kuonyesha utamaduni, mavazi, lugha, chakula nk, zilifanyika siku ya jumamosi tarehe 7/09/2024 ambapo Tanzania pia ilishiriki.
Tanzania iling’ara sana kwenye sherehe hizo ambazo balozi Chipeta aliingia jukwaani katika kuonyesha vazi la asili ya mswahili wa mwambao wa pwani, Tanzania ilionyesha utamaduni wa mtanzania na kuinadi nchi kimataifa kwa kuonyesha vyakula, mavazi na nyimbo. Sherehe hizi ni muhimu na ni fursa kwa nchi kutangaza utalii, biashara, utamaduni na kwa ujumla kama anavyotilia mkazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassana balozi zetu zijikite kwenye Diplomasia ya uchumi.









